Mpendanchi-2
JF-Expert Member
- Apr 4, 2009
- 304
- 38
Huku Nchi ikiwa na matatizo lukuki ya kukosa pesa za huduma kwa jamii uchunguzi uliofanywa unaonekana kuna uzembe mkubwa sana TRA kwa kutotambua baadhi ya kodi na kuzifuatilia na kubaki wakiwakandamiza wafanyakazi kulipa PAYE kubwa ambayo ukusanyaji wake hauna jasho.
Uchunguzi unaonesha kuwa Wamiliki wengi wa majengo , nyumba za kupanga, guest house na hata za makazi hawalipi kodi ( Income tax ) inayotokana na kupangisha watu. Yaani kama mimi nina nyumba nimekupangisha wewe umeweka duka , basi TRA wanafuata yule mwenye duka na kuchukua income tax itokanayo na duka tu, na wala hawahitaji kujua mwenye nyumba pato alilopata kutokana na upangishaji huo amelipa nini !!!
Kuna mifano ya watu wawili nilio nao karibu sana :
1. Ana nyumba pale Kariakoo, of course ni ya urithi ina frame za duka kumi, na kila frame amepangisha 400,000/= kwa mwezi, hivyo anapata 4,000,000/= kwa mwezi kama kodi ya pango kwa wateja wake.
Lakini yeye haijui TRA na wala hajawahi lipa Income tax. Anachojua yeye ni kulipia kodi ya jengo inayolipwa Manispaa kwa mwaka ambayo huwa ni ndogo haizidi 100,000/= kwa mwaka. TRA wakifika wao na wenye maduka tu!!!
2.Mwingine naye ni rafiki yangu na ana nyumba yake pale Ilala , naye ana maduka kama saba hivi, amepangisha 350,000/= kwa mwezi . anapata kama 2,450,000/= Tsh kwa mwezi kutokana na kodi ya pango naye haijui TRA kwenye mambo ya Income Tax.
Na inaonekana ni karibu watu wote wenye nyumba za kupangisha hawaijui TRA , Je haya mapato yanayotokana na upangishaji wa nyumba hayastahiri kulipiwa Income tax??? Kama yanastahiri kwa nini TRA wasichukuliwe hatua kwa kuikosesha mapato Serikali na huku tukiwalipa mishahara minono ili wafanye kazi nzuri.??
Na hili linaweza kuwa hata kwenye mahotel makubwa tunayoyaona ukaona kodi inayofuatwa ni ile ya biashara tu, lakini itokanayo na pango la nyumba usiisikie!!!
Yes, hata mimi kanyumba kangu nimepangisha lakini sijawahi ona nikiulizwa mapato yake ili nilipie kodi. Sasa huu ni uzembe au hakuna sheria ya kodi ya pango.???