Ni kweli mashine za kunyolea saluni huchangia kuenea kwa VVU?

Ni kweli mashine za kunyolea saluni huchangia kuenea kwa VVU?

icon_07

New Member
Joined
May 17, 2023
Posts
3
Reaction score
0
Wazee wa kuzingatia "Angle" uzi huu unawahusu.

Serikali yetu kupitia wizara ya afya imekua ikitumia jitihada kubwa sana katika kuhakikisha maambukizi ya VVU yanapungua nchini. Moja ya jitihada hizo ni utoaji wa elimu kwa jamii namna mbalimbali za kujikinga na maambukizi hayo, mfano kuepuka ngono zembe, na kuepuka kuchangia vifaa vyenye ncha kali kwani vitu hivyo husababisha kwa kiasi kikubwa kuenea kwa maambukizi.
f87340cdb14be9544d2e727a6948e41a.jpg


Ningependa kufahamu ikiwa mashine ya kunyolea ni moja ya vifaa vyenye ncha kali, Je ni kweli mashine za kunyolea saluni husababisha kuenea na maambukizi ya VVU?
Kama jibu ni ndio, kwanini mkazo usiwekwe katika utoaji elimu hususani mashuleni, kwenye vyombo vya habari, na taasisi zingine za umma kuhusiana na matumiz i sahihi ya mashine hizi? kwana sababu kwenye wanaume 100 kuna uwekakano wanaume za zaidi ya 80 wananyoa saluni kwa kutumia mashine za kuchangia. Kama ni kweli nyia hii inaambukiza hamuoni watu wengi tupo kwenye hatari kubwa?

Nimefanya uchunguzi, kwenye saluni 15 unaweza kubahatika kukuta saluni 1 tu ambayo ina sterilizer, tena utakuta imewekwa kama fashion tu, haitumiki ipasavyo kama vile baada ya mtu mmoja kunyolewa.

Ushauri: Kama unajiweza kiuchumi ni bora ukanunua mashine yako binafsi ili unapoenda kunyolewa saluni utumie mashine yako mwenyewe, hii itasaidia kuepuka kupata hata magonjwa mengine kama vile ya ngozi.
 
Back
Top Bottom