Ni kweli mpesa master card inanunua bidhaa mtandaoni?

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Habari wapendwa wana jukwaa napenda kuuliza jee ni kweli kuwa mpesa visa master card inaweza kufanya manunuzi mtandaoni km ebay,aliexpress,na amazon?
Jee vipi kuhusu makato na gharama za huduma?
Kipi bora kati ya kutumia mpesa master card kufanya manunuzi au kutumia visa master card ambazo nimezoea kutumia??

Kipi nafuu na kisichokua na makato mengi na makubwa?
 
Naitumia m pesa master card kulipia matangazo Facebook Kila wiki. Ni nzuri kwa kweli
 
Vipi gharama zake wakat unajisajili wana makato hawa??
hawana. Nenda *150*00# ,chagua lipa kwa m pesa, chagua master card, Kisha create card. Then unairecharge, ( hamishia pesa toka m pesa) , ready for transactions
 
Mzigo huu nimetoka kupokea Nimenunua Ebay na Aliexpress kwakutumia MasterCard ya VODACOM.

INAFANYA POA SANA JAMAA WAMEWAZA MBALI MAANA BANK MPKA UPATE PROCESS ZA PAYPAL UJE UFANYIWE MCHAKATO INSHU KWELI ILA VODACOM UNAJISAJILI MWENYEWE FASTA TU.
 
Naomba kuuliza mkuu.Naweza kutumia hiyo huduma kulipia kampuni za betting za kimataifa kama BETWAY na BET365?
 
mkuu me nataka kuagiza mzingo kwel aliexpress kwa kutumia m pesa mastarcard ila inagoma unaweza kunixaidia jinjisi ya kujaza card number holdername expr date na cvv number make apo kwenye holdername xijui nijaze nn nimeweka majina yangu nilio xajilia line lakin inagoma nielekeze mkuu
 
Nimeagiza mzigo aliexpress kwa voda mastercard,,,,, hakikisha umeweka fedha inayotakiwa katika card kabla ya kujaza hizo cvv etc etc......unaweka hela kupitia *150*00#
 

kunixaidia
xajilia
Xijui

Haupo serious kabisa wewe.

dodge
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…