Ni Kweli Mwamposa anaponya Virusi Vya Ukimwi?

The Boldly

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2017
Posts
2,377
Reaction score
5,147
Wakuu habari!

Nilikuwa sehemu fulani jirani yetu kuna watu wengi wamekusanyika wanamuangalia Mchungaji Mwamposa kwenye TV.

Mara nasikia kuna mdada anatoa ushuhuda kuwa ameponywa V.V.U Kabisa.

Hili suala la Mwamposa kuponya V.V.U kwangu naona ni uongo wa mchana kweupe.

Au ni kweli??

Kwamba V.V.U inaombewa na kupotea kabisa?
 
Anaponya kutumia mafuta ya diesel
 
akili za kuambiwa changanya na zakwako....hivyo nenda kajaribu usipopona basi....ila ukipona kaa chini umshuru Mungu
 
Mambo ya kiroho huenda kwa Imani zaidi.
 
Kuna mshkaji tumemzika last year, Mwamposa kamdanganya kapona HIV, akaacha dozi, aisee Ni hatari kusimulia, Kwanza alianza kuumwa kichwaaa, ikaja akarukwa na akili, baada ya hapo kifo
 
Kuna mshkaji tumemzika last year, Mwamposa kamdanganya kapona HIV, akaacha dozi, aisee Ni hatari kusimulia, Kwanza alianza kuumwa kichwaaa, ikaja akarukwa na akili, baada ya hapo kifo
Ni hatari tupu...

Baada ya kuombewa hakwenda kupima?
 
Mwamposa aponye ukimwi yeye ni nani? Yesu ndie mponyaji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…