Ni kweli nchi haina wataalam wa madini?

Ni kweli nchi haina wataalam wa madini?

kifupi kirefu

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2018
Posts
539
Reaction score
3,507
Baraza la mawaziri la Sasa limepata changamoto na ukosoaji mkubwa kwa mambo makuu matano;
1. Halina Waziri full kutoka Zanzibar
2. Halina uwiano wa jinsia
3. Linatuumiwa kuhusu udini na ukanda
4. Wabunge wakuteuliwa kuingia kwenye baraza huku wakiwemo wabunge zaidi ya 300 wamajimbo ambao wameachwa.
5. Lipo tatizo la mawaziri kupewa wizara zilizokinyume na taaluma zao na ambazo hawana uzoefu nazo. Mfano Leo tumeambiwa Waziri wa madini mwalimu, lakini kiuzoefu hajawahi kufanya kazi kwenye hi sekta.

Je, tukiacha sifa 4 za juu, nchi inakosa wasomi na wataalu wakuongoza hizi sekta? Hatuna wataalamu wa madini? Mageologist akina Muhongo ni kwamba hawana uwezo au njia yakupata wateule ni kwa wakubwa kuamua Nani ni mtaalam nani siye?

Kama hatuna wataalamu je hii sekta tunasemaje inafanya vizuri? Ni akina Nani wanaifanya ifanye vizuri? Je hatuoni kwamba mabeberu tulikua tunawasingizia kumbe walikuja wakakuta hatuna wataalamu na Hadi Sasa wanatugharagaza kwa sababu hatuna wataalamu!?
 
Muhongo alikua anafaa sana kwenye hiyo sekta. Wakati ule alifeli maana wizara ilikua kubwa sana maana iliunganishwa na nishati but now angeimudu vema kabisa.
 
Tatizo la Muhongo alikuwa maneno mengi bila matokeo, ss mzee anataka matokeo cyo maneno.
 
Mfano kasekenya kupelekwa ujenzi badara ya madini hata mimi cjaona mantiki ya kuteua wabunge wasomi hafu wanaperekwa kusiko.

Ama kweli nibora ufate ushauri wa mwerevu mwenye mashaka kuliko mjinga anayejiamini.
 
Katiba haikutoa muongozo wa kitaaluma kwenye kuunda serikali..... Kuanzia Rais anaweza kutoka taaluma yoyote ....so hata baraza lake ni hivyo hivyo.... Haikulazimisha mawaziri kutoka pande zote mbili ....na ndio maana hujawahi kusikia baraza la Zanzibar kuna aliyetoka bara. Pia haikuelekeza mlinganyo wa jinsia ....kwa kuwa nafasi hizo sio za kudumu.

Tafakari kabla ya kutoa maamuzi
 
Ukichunguza kwa makini Jpm anajua kubalance ,waziri au naibu waziri utakuta ni mtaalamu wa hiyo sector,kuna mambo mengine ya kiutendaji yanaitaji taaluma zingine zichukue nafasi kubwa
 
Back
Top Bottom