Ni kweli Robertihno kocha?

ESPRESSO COFFEE

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2014
Posts
6,170
Reaction score
7,665
Kuna Vitu Vinafikirisha Sanaa, hasa Ukiangalia Namna Kocha Mkuu wa Simba anavyo ongoza Timu. Nahisi Kocha Wa Simba Anabebwa na Matokeo zaidi kuliko uwezo wake. Najiuliza Maswali Mengi sana

1. Kwanini Kocha wa Simba Anacheza Na Timu as If ina Wachezaji 11 tuu? Kwanini Hafanyi Rotation ya Wachezaji Pamoja na Utitili wa Mechi tulizo nazo?

2. Ndani ya Mwezi wa 10 Simba Imecheza Mechi 6, Mechi za Karibu zaidi ni za Tarehe 20, 24, 28 na Tarehe 05 katika hizi mechi 4 Kocha ameanza na kikosi kile kile, Na Sub Zile zile bila kujari anacheza na nani? Hapa sio Kwamba Kuna Ulakini wa Mbinu?

3. Mechi ya Leo, Kwa Kocha Mwenye Akili Timamu unawezaje Kumuingiza Aishi Manula Ambaye alikuwa majeruhi kwa Muda wa Zaidi ya Miezi 3 halafu unakuja kumuweka Direct kwenye Derby? Yalikuwa maelekezo ya Viongozi au ni Mahitaji ya Kocha? Nje una Ayoub na Una Salim.

4. Saido Alionekana Kuchemsha hii mechi toka Kipindi cha Kwanza, Kwa Kocha mwenye Uwezo unawezaje Kumuacha huyu mchezaji amalize Dakila 90?

5. Inakuwaje kwa wewe kocha Ambaye ni mtaalamu, Timu inatatizo la Beki za Kati kwa miezi 6 sasa, na Hakuna Improvement, Kwanini Usiwajaribu mabeki wengine ulio nao benchi?

6. Kapombe na Zimbwe kwa macho ya kawaida wanaonekana wamechoka, Angalia Magoli ya Leo yaliko tokea, Lakini Kwanini Kocha Umeendelea kuwa King’ang’anizi?

7. Unacho Mpendea Baleke Kwenye Derby ni Nini? Unaogopa kwasababu Phiri hana Rotation nzuri kwenye Kikosi? Baleke Kama Saido na Chama hawako vizuri Baleke ni Pazia tuuu, Kama Kapombe na Zimbwe Hawapigi Cross Baleke Hana Faida Mbele ya Phiri

8. Kama Kocha Kwanini huwaambii wachezaji waachr kurogana? Kramo Angekuwa Mbali Kiasi Gani?

9. Sijaona Mbinu wala Falsafa Ya Mpira wa Robertihno zaidi ya Juhudi Binafsi za Wachezaji.

10. Viongozi wa Simba Kama Mtaenda na Robertihno Makundi ya CAF CL sitashangaa tukiishia hatua ya Makundi.

TUSHINDE AU TUFUNGWE ROBERTIHNO SIO KOCHA SAHIHI WA SIMBA HASA HII yenye wachezaji wengi Wazuri
 
Shida ya simba ni kocha kasongo athman alisema so kocha na wadau kibao wakampa mileage eti hajawahi kupoteza mechi tangu aingie nchini huku timu Ina struggle sana sana kila mechi inaruhusu goli ulikuwa wake up call wakaona acha waone Leo ndio wameona
 
"Kocha ameanza na kikosi kile kile, Na Sub Zile zile bila kujari anacheza na nani? ""
Nimeishia kusoma sentesi hii... kocha na wewe wote vilaza sijui kuhusu wachezaji...
 
Yaweeeee kumbe ule ukuta wa yeriko ni mbwembweee🤭🤭😅😅
 
Plan B ya kikosi chetu cha simba hakuna. Wachezaji wale wale
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…