sun wu
JF-Expert Member
- Apr 1, 2012
- 2,020
- 1,422
Ni mengi yamesemwa kwamba tumekuwa watumwa kwa kuchukua lugha za kigeni na Kikoloni.., wengine wamefikia hatua ya kusema kwamba kwanini Kiswahili kinatumika mpaka darasa la saba na kwanini kisiendelee kutumika hadi O-level na A-level kufundishia..?
Mimi ninakubaliana nao kwa masomo kama Historia; General Studies, na Jiografia, lakini tusifanye makosa ya kutaka kutafsiri masomo ya Sayansi na masomo mengine ambayo chipuko lake na theories nyingi zipo kwenye Kingereza., sababu hapo inaweza kutokea (Lost in Translation) na kupoteza maana ya maneno na kuwachanganya watu badala ya kuwafundisha. Ukizingatia vitabu vingi na documentantion nyingi zipo kwenye Kingereza na kubadilisha lugha kunaweza kuwafanya wanafunzi kuwa at a disadvantage ya kupata materials na zile ambazo lugha imebadilishwa ufanisi huenda usiwepo
Mpaka pale tutakapoanza kuandika vitabu vingi kwa Kiswahili na ugunduzi mwingi kufanywa na waswahili ndio labda tuanze kufikiria hili jambo lakini kwa sasa tutakuwa tunaharibu badala ya kujenga