Sanitaiza
Member
- May 19, 2020
- 30
- 21
Wakuu habarini za wakati, wanaboard.
Moja kwa moja nijikite kwenye mada. Nimefuga kuku kwa miaka takribani 6 sasa. Nimefuga kuku wa mayai (layers) na kuku wa nyama (broilers). Katika ufugaji wangu nimezingatia kanuni zote pamoja na ushauri wa wataalam.
Nimekuwa nikipata matokeo chanya katika miradi yangu. Kwa kweli ni jambo la kumshukuru Mungu.
Sasa wakuu, changamoto inakuja kwenye soko. Kuna wale jamaa wanakuja kununua kuku wa nyama usiku usiku mida ya sa 9 au sa 10 alfajiri. Kwa jina maarufu wanaitwa watu wa matenga. Hawa jamaa wanaweza nunua kuku hata 200 wa nyama na wanakupa hela yako vizuri. Kimbembe sasa njo asubuhi hesabu kuku waliobaki, utakuta wamebaki kuku wachache sana. Wengine wamekupiga.
Wakati mnauziana huwa hawapakizi mpaka na wewe uone ndio uruhus wapakize. Kwa kifupi mnahesabiana vizur tu. Ila ambacho sielew huwa wakija kununua kuku lazima waje na kuku wao wachache kama 10 hivi wako kwenye kirikuu.
Sasa sielewi huu uchawi au mazingaumbwe.
Ni kweli tutatoka kwa hii style au ndio tunapoteza muda.
Kwenu wadau, naombeni ushauri, nifanyeje ili niwadhibit hawa jamaa kwenye biashara yangu.
Asanteni wakulu