SoC02 Ni kweli unaona ilivyo?

SoC02 Ni kweli unaona ilivyo?

Stories of Change - 2022 Competition

MASTER 01

New Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
1
Reaction score
0
MACHO ni sehemu ya mwili inayotuwezesha kuziona taswira zetu zilizondani kwa nje, kile kinachoonekana ni taswira ya kitu namna tunavyokitafsiri katika akili zetu.

Tunaona tulivyo sio kama vitu vilivyo ndio maana ukizidisha umakini wa kuangalia kitu unaweza ona kitu kingine tofauti na taswira ya mwanzo uliyokuwa nayo.

Kama macho yakifumbwa taswira inaweza kupotea katika macho ila akilini hubaki sababu taswira hutengenezwa na milango yote ya fahamu.

Ukitumia milango yote ya fahamu unaweza ona vizuri zaidi tofauti na macho pekee, Huoni nje ila unaona taswira ulizonazo ndani.

Unaweza Jenga taswira kwa kuona, kunusa, kugusa, kulamba na kusikia.

Macho yanaweza Jenga taswira za vitu vya nje zaidi tofauti na milango mingine ya fahamu hasa kukiwa na mwanga,
bila mwanga huwezi kuona hata kama macho hayajafumba

Japo kuna hali inaweza pelekea usione hata kama hujafumba macho kama akili ikawa inafanya kazi zaidi na kujenga taswira za vitu ambavyo havipo mbele ya macho.

Macho husaidiana na akili (intellect) kutafsiri vitu kwa namna tulivyovijua, kuambiwa na kufundishwa toka utotoni.

Cobra (nyoka) Hana macho ila anauwezo wa kuhisi tetemeko la ardhi lililombali sana hivyo Kama ukijifunza kutumia milango yote mitano ya fahamu unaweza ona vizuri zaidi ya mtu mwenye Macho .

Sio kila mwenye macho anaona.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom