MTWA
JF-Expert Member
- Aug 5, 2009
- 1,166
- 168
Ndugu wana JF
Mimi binafsi sijafurahishwa na vile Mkutano Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ulivyotumika kuwananga viongozi na wanachama wa vyama vya siasa kwa kuitwa mavuvuzela.
Vuvuzela ni aina ya tarumbeta zinazotumika katika kushangilia timu zinazoshiriki katika fainali za kombe la dunia zinazofikia kilele chake hivi karibuni. kwa timu za Taifa za Hispania na Uholanzi.
Wakati wapinzani wakiitwa mavuvuzela, viongozi wake wakuu akiwemo Profesa Ibrahim Lipumba (Mwenyekiti wa CUF), Augustine Mrema (Mwenyekiti wa TLP) na Said Arfi (Makamu Mwenyekiti wa Chadema) walikuwemo ukumbini Kizota mjini Dodoma.
Pia walikuwepo viongozi kutoka vyama vya upinzani vya NCCR-Mageuzi, UMD, SAU, Demokrasia Makini, NRA, AFP, NLD, APPT, UPDP, Tadea) na UDP.
Waliotoa tamko hilo ni wanafunzi wa Vyuo Vikuu walio wanachama wa CCM, wakati wakiimba na kuwasilisha salamu zao kwa wajumbe wa mkutano huo.
Wakati wakiimba wimbo maalum, miongoni mwa maneno yaliyotamkwa ni mwaka huu tutawacharaza wapinzani, tuwape adabu, tuwapige kwa kura ya ndiyo shika kura yako juu, tandika sawasawa mavuvuzela hao hawatuwezi,
SASA JE KAMA HII NDO TANZANIA TUTAKUJA FIKA WAKATI TUKAKOMBOLEWA NA HII HALI TULIYONAYO?