Wana JF naomba kama kuna mwenye uhakika. Nimepata tetesi kuwa baadhi ya vyuo vikuu ambavyo wanafunzi wake tuko likizo fupi ya kumaliza semester 1 vitachelewa kwa kuwa loan board haina hela za kutupa kumalizia huu mwaka. Mi niko kijijini. Naomba kama kuna mwenye uhakika anijulishe vizuri nisijechoma nauli yangu bure.
Hizo taarifa zipo, na inavyoonekana zitaathiri zaidi hivyi vyuo vya kubandika kwa Plasta kwana wapigania haki wa UDSM wameshapata chao, So ndugu wewe jiandae kwa lolote lile!!