Ni kweli Waafrika hatukuwa na Historia kabla ya ujio wa Wazungu?

Kwamba Waafrika hatukuwa na historia yetu kabla ya ujio wa Wazungu ni uzushi mkongwe. Uzushi huu ulianza karne ya 19 na kushamiri hadi karne ya 20. Hiki lilikuwa ni kipindi cha ubepari mkongwe au ubeberu (imperialism) ambapo mabepari wa Ulaya walieneza na kuupa nguvu uvumi huu ili kuwadunisha Waafrika na kuwafanya watawalike kirahisi.

Kigezo kikubwa kilichotumika katika madai haya ni kuwa historia huhifadhiwa katika maandishi (written documents) na Waafrika hawakuwa wameandika kuhusu historia yao. Maandishi katika Africa yameletwa na mtu mweupe wakati wa ukoloni.

Ukweli ni kwamba kila jamii ina namna yake ya kuhifadhi historia na kumbukumbu nyingine muhimu. Kwa hiyo kiasi kikubwa cha historia ya Waafrika kilihifadhiwa katika masimulizi ya mdomo (oral traditions). Pia tafiti nyingi za akiolojia (archaeological studies) zimeonyesha kwamba Waafrika wanayo historia kuongea. Imethibitika pasipo shaka yoyote, kwa mfano, kwamba ajili ya binadamu ni Afrika. Imethibitika pia kuwa ni Waafrika ndio walioanza kujenga waliojenga Mawe Zimbambwe? Au kuhusu ajili ya ufaidi chumba katika Africa?
 
Upo sahihi, kwa mfano hai mimi binafsi nimesoma historia ya kabila langu lakini mwandidhi wa kitabu karibu historia yote muhimu amecopy maandishi ya wazungu wa kwanza kufika katika eneo letu ambapo maandishi hayo yamehifadhiwa kwenye ofisi ya mkuu wa mkoa, hawa wazungu walikuwa wakisimuliwa na babu zetu na wao wakawa wanahifadhi kimaandishi, utata je waliandika kweli tupu? Tumeshapigwa bao na wazungu.

Cha msingi ni sisi waafrika kuipekuwa historia ya kweli ya wazungu na sivyo walivyotuandika sisi je waliwezaje kutuzidi akili?
 
Jielimishe. Hata mwanafunzi wa historia wa darasa la nne anafahamu vema
 
Hii ni mada nzuri sana, Afrika ilikua na historia na hii ipo dhahiri. Licha ya kwamba elimu yetu inaonesha kwamba historia huandikwa lakini tunasahaulishwa vyanzo vingine vya historia.
Historia ni mtindo wa maisha na hudhihirishwa kupitia mtindo wa maisha kisiasa, uchumi na jamii vilevile sayansi na teknolojia. Uthibitishe wa kuwepo kwa historia upo kupitia mambo kadhaa ambayo yalipenya misukosuko ya wageni, utunwa na kutawaliwa.
Tukiabgalia imani za asili, kazi za sanaa, mitindo ya ujenzi, utawala, matibabu na mengine mengi ni uthibitisho wa historia ya Afrika kabla ya kuingiliwa. Ningeeleza zaidi ila nipo kazini hapa!
 
Haya tunayathibitishaje?
Historia iliikuwepo ila haikuandiikwa, hao wazungu walipokuja Afrika walikuta ardhi tupu bila watu, na kama waliwakuta watu pia waliwakuta watu wazima ambao ambao tayari walikua wamefanya meengi, kwako wewe mkuu historia nini?
 
 
Waafrika wana historia na falsafa tatizo ni matokeo ya utumwa yalifuta kila kitu kilichokuwa ni utambulisho wa muafrika. Kwa utafiti naoendelea kuufanya unathibitisha waafrika walikuwepo tena kabla ya adam na hawa, nitaiwasilisha ripoti kamili itapokamilika ila tambua Afrika was mother of civilization
 


Fufu la Binadamu wa kwanza karne hii wapi inapatikana?. Kama kweli Biandamu wa kwanza kaanzia Tz kwanini tuko nyuma kiasi hiki hata Afrika?.


Olduvai Gorge - Wikipedia, kamusi elezo huru

Kwa kuwa watu wanadhaniwa kutokana nao, eneo hilo pengine limeitwa kwa Kiingereza Cradle of Mankind, kitovu cha binadamu, ambao wameishi katika eneo hilo kwa walau miaka 17,000 mfululizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…