Ni kweli wafungwa wanakula mlo mmoja kwa siku na ni haki?

Viva89

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2012
Posts
1,261
Reaction score
528
Jamani,hawa watu sawa weonekana kufanya makosa in the society,ila ni haki kweli kumpa mlo mmoja kwa siku kama inavyosikika kwa sababu ni mfungwa? Zitto Kabwe aliuliza swali la ukweli,"wafungwa na mahabusu wanapata chakula mara ngapi kwa siku?"..hawa watu huwa wanasaulika kabisaaa,ila wanahaki zao pia,including kwenye kula,malazi na kadhalika,au wanaJF mnaonaje?ni haki mlo mmoja kwa siku?
 
Ni kweli hali ya wafungwa na mahabusu ni mbaya sana na wengi kama si wote wanakula mlo mmoja...Ila kwa taratibu za nchi hii ni vigumu kuwahoji wahusika kwa sababu suala la wafungwa na magereza liko chini ya jeshi la magereza sana sana utakachoambulia ni "MAMBO YA JESHI HAYAHOJIWI PUBLICALLY"
 
Uji saa 5 na chakula saa 9...siku imepita!!
 
dah!..sasa inamaanisha hawawezi rekebisha?wapi watu wa human rights?!!!...
 
wanaenda kutengeneza vitambi kule? soon utaskia wapewe bia na thoda.
 
kitaa watu wanashida wengne wanakula mara moja no uji, wakiweia hyi mara tatu usishangae gereza zikafurika
 
Kitaalamu mfungwa anakula mara tatu kwa siku. Uji asubuhi na mchana mara moja lakini mlo wao unajumuisha na wa usiku. Mfano, kama mchana anakula robo na jioni robo kilo basi anapewa nusu kilo kwa mlo wa mchana kama compasation ya chakula cha usiku.

Hiyo stori niliwahi kuisikia kwa hao jamaa wanaojiita wajelajela gwaaa.
 
Mkuu, usishangae hilo. Nchi hii watu wanakula mpaka pesa za waathirika wa Ukimwi, yatima na pesa ya chakula ktk hospitali. Mimi nimewahi kutembelea mgonjwa pale Muhimbili, chakula alichopewa kilinisikitisha. Tunatesana sisi kwa sisi. Magereza nafahamu bajeti zao zinaonesha milo mitatu, ikiwa pamoja na ratiba za nyama, matunda, maziwa nk. Na haya malipo hufanyika na serikali. Swali ni je hali ndiyo hiyo?
 
dah,tunahitaji kubadilika aisee...maneno yako yamenigusa na kunisikitisha mkuu..aibu!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…