Ni kweli wakulima wa kahawa Uganda wananeemeka kuliko wenzao wa Tanzania?

Ni kweli wakulima wa kahawa Uganda wananeemeka kuliko wenzao wa Tanzania?

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,189
Reaction score
10,375
Tanzania ina ardhi kubwa kuliko Uganda, lakini kuna watu wa Bukoba wanaotamani wangekuwa wanaenda kuiuza kahawa yao nchini Uganda.

Tanzania inayo bandari, lakini Mganda akitaka kusafirisha kahawa yake, kama siyo kwa ndege, basi atalazimika kuitumia bandari ya Tanzania au ya Kenya.

Pamoja na hayo, bado kuna Watanzania wanaotamani wakaiuzie kahwa yao nchini Uganda. Hiyo inaonesha kuwa wakulima wa kahawa nchini Uganda wanafaidi zaidi kuzidi wa upande wa Tanzania.

Huo utofauti umetokana na nini?
 
Broo mazao haya makubwa katani , kahawa , chai pamoja pamba ni mazao ambayo huiinua uchumi wa mkulima na nchi kwa haraka sana , sasa penda usipende kuna watu wanaidhofisha ili Tz isinufaike nayo kuanzia maswala ya bei pamoja na masoko yake...
 
Na sijawahi kusikia wala kuona kahawa inaingizwa kimagendo kutoka Uganda kuja tanzania kuuza

Ova
Na mimi ndiyo nataka kufahamu, kwa sababu, kwa Jiografia ya Uganda na Tanzania, ni Waganda ndiyo walipaswa wawe wanakuja kuiuza kahawa yao Tanzania. Lakini pamoja na kwamba wao hawakatazwi kuileta Tanzania, hawafanyi hivyo.
 
Inaonkeana bei inayopatikana Tanzania ni ndogo kuliko Uganda.
Hiyo ni failure ya bodi ya Kahawa na Wizara ya Kilimo kwa ujumla.
Kuna watu walipaswa wasiwepo kwenye nafasi zao,wanaihujumu nchi
 
Back
Top Bottom