Elections 2010 Ni kweli waliojiandikisha kupiga kura zaidi ya watanzania milioni 19?

Elections 2010 Ni kweli waliojiandikisha kupiga kura zaidi ya watanzania milioni 19?

Dullo

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2009
Posts
251
Reaction score
64
WanaJF mie ninapata mashaka kama kweli katika nchi yeyote nusu ya watu wake wakawa wamejiandikisha kupiga kura, maana tunaambiwa Watanzania tunakadiriwa kufikia milioni 40 huku vijana wakikadiriwa kuwa ni zaidi ya asilimia 60 watoto sijui ni asilimia ngapi na wazee pia.

Hebu tusaidiane kupena data hizi kuhusu idadi iliyotolewa ya hawa wapiga kura mwaka huu.

Niko njia panda nifafanulieni.
 
Idadi ya watanzania kwa sensa ya mwaka 2002 ni 34,859,582 na kati ya hawa 17,775,733 au 51% walikuwa wana umri wa miaka 0-17. Ina maana kuwa waliokuwa na umri wa miaka 18 na kuendelea ni 17,083,849 au 49%. Makisio ya idadi ya watanzania kwa mwaka 2010 ni 43,187,823 na kati ya hawa, inakisiwa kuna watanzania 21,165,321 au 49 % wana umri wa miaka 18 na kuendelea, na hawa ndio wapiga kura watarajiwa. Hivyo basi, NEC inasema imeandikisha watanzania 19,000,000 na hii ni kama 90 % ya walengwa!!! Naona hapa NEC haijakosea, lakini je kulikuwa na mwamko mkubwa kiasi cha kuwezesha watanzania wote wa umri wa miaka 18 na kuendelea kuandikishwa?! Kazi iliyoko mbele yetu ni kuhamasisha ndugu na jamaa zetu siku ya kupiga kura waende wakapige kura kwa mgombea udiwani, ubunge na uraisi wanayeona atawafaa kwa miaka 5 ijayo, siyo yule aliyewapa zawadi, chakula, nguo na kadhalika wakati wa kampeni.
 
Possible kwasababu wengi walijiandikisha uraia ukizingatia hatuna vyeti vya uraia. sehemu nyingi ukienda walikuwa wanaomba vyeti vya kupigia kura kama utambulisho wa uraia ndo maana watu wengi walijiandikisha.
 
nadhani hapa kuna tofauti ya kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura na kupiga kura, inawezekana kabisa ni kweli hao watu wamejiandikisha kwa minajili ya kupata kile kikadi cha kura ili wakitumie kwenye mambo yao kama utambulisho wa utanzania, Lakini inavyoonekana tume ya uchaguzi inataka kutumia hiyo list kujustfy wizi unaotarajiwa kufanyika
 
Hesabu inaweza kuwa kweli lakini tatizo likawa kama ambavyo Kituko amesema maana matumizi ya hizi kadi ni mengi zaidi ya kupiga kura.
 
Asanteni kwa kunisaidia huu ufafanuzi hasa kwa ule Mama Mdogo, Thanx.
 
Maoni yangu ni kwamba, humu Jf kuna watu wana JF ac zaidi ya Moja!. Mtu anaanzisha thread kwa ac fulani, halafu anaijibu kwa ac nyingine, lengo likiwa ni kupotosha umma. Ukweli ni kwamba hakuna uwezekano wa watu waliojiandikisha kufikia hiyo mil 19 laki 6 almost mil 20. This is next to impossible!!. Kwa literacy level ya TZ, Miundombinu yote ya uandikishaji na mengineyo. Yaani inakaribia 100%. Shame on you NEC. Kaeni mkijua ipo siku Mungu atawahukumu kwa hujuma hii mnayowafanyia watanzania!!.
 
kazi kweli kweli ... mimi nasubiria kuona namna ccm watapull this one off
 
Kwa nchi zinazoendelea hususani Tz ni vigumu sana kuandikisha kwa 90% ya walengwa wote,mbona Zanzibar idadi ya wapiga kura safari hii ni ndogo kuliko mwaka 2005?Inakuwaje huku bara kuwe na ufanisi kihivyo?Hii ni janja ya kuchakachua matokeo.Ila malalamiko ya watanzania hayatoenda bure,Mungu yupo anasikia.Sisi tufanye sehemu yetu,kupiga kura na kuzilinda.
 
Maoni yangu ni kwamba, humu Jf kuna watu wana JF ac zaidi ya Moja!. Mtu anaanzisha thread kwa ac fulani, halafu anaijibu kwa ac nyingine, lengo likiwa ni kupotosha umma. Ukweli ni kwamba hakuna uwezekano wa watu waliojiandikisha kufikia hiyo mil 19 laki 6 almost mil 20. This is next to impossible!!. Kwa literacy level ya TZ, Miundombinu yote ya uandikishaji na mengineyo. Yaani inakaribia 100%. Shame on you NEC. Kaeni mkijua ipo siku Mungu atawahukumu kwa hujuma hii mnayowafanyia watanzania!!.
may be ur right
 
Back
Top Bottom