Idadi ya watanzania kwa sensa ya mwaka 2002 ni 34,859,582 na kati ya hawa 17,775,733 au 51% walikuwa wana umri wa miaka 0-17. Ina maana kuwa waliokuwa na umri wa miaka 18 na kuendelea ni 17,083,849 au 49%. Makisio ya idadi ya watanzania kwa mwaka 2010 ni 43,187,823 na kati ya hawa, inakisiwa kuna watanzania 21,165,321 au 49 % wana umri wa miaka 18 na kuendelea, na hawa ndio wapiga kura watarajiwa. Hivyo basi, NEC inasema imeandikisha watanzania 19,000,000 na hii ni kama 90 % ya walengwa!!! Naona hapa NEC haijakosea, lakini je kulikuwa na mwamko mkubwa kiasi cha kuwezesha watanzania wote wa umri wa miaka 18 na kuendelea kuandikishwa?! Kazi iliyoko mbele yetu ni kuhamasisha ndugu na jamaa zetu siku ya kupiga kura waende wakapige kura kwa mgombea udiwani, ubunge na uraisi wanayeona atawafaa kwa miaka 5 ijayo, siyo yule aliyewapa zawadi, chakula, nguo na kadhalika wakati wa kampeni.