Jamani naomba ufafanuzi juu ya hili jambo ambalo nimelisikia
hivi karibuni, eti wanaume wenye maumbile makubwa wana
uwezekano mkubwa zaidi wa kuambukizwa au kuambukiza
magonjwa ya zinaa hususani UKIMWI kuliko wale wenye
maumbile madogo?
Eti wanaume wenye maumbile madogo wana nafasi ya
kunusurika kwa asilimia kubwa kuambukiza au kuambukizwa?
Swali lako mwanangu gumu. Linahitaji utafiti wa kina na siyo kuhisi wala kukurupuka. Hata hivyo magonjwa ya zinaa yanawapata wazinzi sana kuliko wale wasiozini wawe na maumbile makubwa au madogo.
Swali lake ni zuri sana ambalo linahitaji majibu ya kitaalam, nashangaa wanaomshambulia.Kumbukeni kuna prof. kama sikosei ni Kenya alitafiti na kugundua wanaume waliotahiriwa wana uwezekano mdogo wa kuambukizwa ukimwi kuliko ambao hawajatahiriwa.Ingawa ni tofauti na swali la mleta mada lakini unaweza pata picha jinsi haya mambo ya kisayansi yasivyohitaji kukurupuka.Wataalam mtusaidie.