Ni kweli wataalamu wa Jadi wanatoa msaada katika Jamii au ni Utapeli?

Ni kweli wataalamu wa Jadi wanatoa msaada katika Jamii au ni Utapeli?

Kaunara

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2013
Posts
249
Reaction score
452
Wataalamu wa jadi wapo dunia nzima kila sehemu wapo.

Katika maisha ya binadamu kuna mauza uza mengi sana. Kuna mda binadamu anashindwa kupata hata usingizi kutokona na mambo kuwa tight. Kila mmoja anajua ni jinsi gani anajua kutatua changomoto kama hizi wengine wanamalizia stress na pombe, wengine kanisan, wengine kwa marafiki wengine kwa wataalamu hawa wa jadi wengine wanakufa nazo ndani tu kila mmoja anajua ni wapi anamalizia stress zake.

Swali langu ni hawa ambao wanachangamoto ambazo wanazipeleka kwa wataalamu wa Jadi, je ni kweli uwa wanapata msaada kutoka kwa hawa watu?

kuna madhara yeyote ambayo wamepata kutoka kwa hawa watu? wakati wakipata msaada au baada ya msaada kupata?

Soma Pia: Tuwaheshimu Watalamu wa Jadi

Karibuni.
 
Nawekaa nanga wataalamu waje waweke sawa
 
Tatizo,watu wengi mnapendaga kujifunga akili.
1. Kabla ya haya sijui ya Mungu na Yesu na Maria(uzuri watu wazima wa umri kama 90 hivi)wana ushahidi.

2. Tatizo la hawa wa kisasa,ni wahuni wahuni tu. Utasikia lete kwanza elfu 30,jambo lako gumu. Ikishafika laki,bado unaona kuacha huwezi,na kuendelea unashindwa. Sasa hivi,wengi matapeli. Mtaalamu wa kweli hawezi chukua zaidi ya buku 2. Na anakwambia malipo ni baada ya huduma.

Kipindi furani nilikuwa mi siamini uwepo wa haya mambo. Nilikuja kushuhudia jama ana kama kifafa hivi,lakini akianguka,paka wanalia tumboni mwake mpaka basi. Ikasemekana(kwa wanaomjua na waliokwishamzoea),kwamba alifanyiziwa na ndugu zake.
Kama hujakumbana nalo,hata hutohangaika kujua kama kweli yapo au ni uongo
 
Back
Top Bottom