Ni lazima kupata kibali cha ujenzi kabla hujaanza kujenga nyumba ya makazi?

kimara Kimara

Member
Joined
Jul 7, 2024
Posts
80
Reaction score
173
Moja kwa moja kwenye mada, Nauliza ni lazima upate kibali cha ujenzi ndipo uanze kujenga ? Na hiko kibali kinapatikana wapi, Gharama yake kiasi gani, umuhimu wa hiko kibali,

Naomba maelekezo zaidi jamani mliowahi kujenga .
 
Ndiyo, ni LAZIMA, ingawaje Sheria zinatungwa ili zivunjwe.
Eneo lako limepimwa? Tuanzie hapo kwanza
Hata kama eneo au Ardhi husika bado haijapimwa, kupata Kibali cha Ujenzi ni LAZIMA. Hilo ni takwa la kisheria.
Sheria zinatamka kwamba Mwombaji wa Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni LAZIMA awe Mmiliki halali wa ARDHI ambayo ujenzi husika untakiwa kufanyika.
Aidha, ukisoma tafsiri ya kisheria ya neno "ARDHI" kwenye Sheria za Ardhi, utaona kwamba imeelezea aina zote kabisa za Ardhi kwa ujumla wake, yaani imejumuisha Ardhi iliyopimwa (surveyed land) na Ardhi isiyopimwa (unsurveyed land), Sheria hazijatenganisha kuhusu suala hili kwamba Kibali cha Ujenzi kinatakiwa kuombwa kwenye Ujenzi unaofanyika kwenye Ardhi iliyopimwa tu peke yake.
 
Moja kwa moja kwenye mada, Nauliza ni lazima upate kibali cha ujenzi ndipo uanze kujenga ? Na hiko kibali kinapatikana wapi, Gharama yake kiasi gani, umuhimu wa hiko kibali,

Naomba maelekezo zaidi jamani mliowahi kujenga .
1. Ni lazima kupata kibali cha ujenzi kwa sheria zetu
2. Kibali kinapatikana halmashauri ya mji husika
3. gharama ni 200k kwa maeneo yasiyopimwa, kama pamepimwa ni kwa square meter za jengo,
4. umuhimu ni kujihakikishia usalama wa jengo lako na kukuwezesha kupata mkopo kwenye taasisi za kifedha na pia husaidia kuepusha migogoro ya ardhi. LAITI kama kila anaejenga atafata kanuni zote za kupata kibali cha ujenzi basi itasaidia sana kuondoa kero ya migogoro ya ardhi.
 
1. Uko sahihi, kupata Kibali cha Ujenzi ni suala la LAZIMA kwa mujibu wa Sheria za nchi.
2. Uko sahihi pia, Kibali cha Ujenzi utakipata kutoka Ofisi za Halmashauri ya Wilaya, Mji, Manispaa au Jiji.
3. Sidhani kama utakuwa uko sahihi.
Gharama hutegemeana na sababu mbalimbali, kama vile: Mahali pa ujenzi, ukubwa wa jengo linalotakiwa kujengwa, hali ya Ardhi yenyewe, Soil Investigation Report, or EIA Reports, n.k, n.k.
4. Yes, kwa kiasi fulani Kibali cha Ujenzi kinasaidia kuondoa au kuepusha migogoro ya Ardhi.
Aidha, Vibali vya Ujenzi pia husaidia katika Kudhibiti Ujenzi holela usiokidhi Viwango Bora vya Kiusalama kwa Wakaazi.
 
Yes kwenye gharama sijaweka details zote...nime assume kwa DSM Ili apate picha,
 
Ndiyo, ni LAZIMA, ingawaje Sheria zinatungwa ili zivunjwe.

Hata kama eneo au Ardhi husika bado haijapimwa, kupata Kibali cha Ujenzi ni LAZIMA. Hilo ni takwa la kisheria.
Sheria zinatamka kwamba Mwombaji wa Kibali cha Ujenzi (Building Permit) ni LAZIMA awe Mmiliki halali wa ARDHI ambayo ujenzi husika untakiwa kufanyika.
Aidha, ukisoma tafsiri ya kisheria ya neno "ARDHI" kwenye Sheria za Ardhi, utaona kwamba imeelezea aina zote kabisa za Ardhi kwa ujumla wake, yaani imejumuisha Ardhi iliyopimwa (surveyed land) na Ardhi isiyopimwa (unsurveyed land), Sheria hazijatenganisha kuhusu suala hili kwamba Kibali cha Ujenzi kinatakiwa kuombwa kwenye Ujenzi unaofanyika kwenye Ardhi iliyopimwa tu peke yake.
Urasimu ndiyo kikwazo kikubwa kwa wengi, gharama ya kupata kibali (mlungura) ni kubwa kuliko matazamio
 
Usisahau na yafuatayo:-
1-Kibali cha kuhamia nyumba yako mwenyewe kutoka kwenye mamlaka husika umalizapo ujenzi na kutaka kuhamia.
2-kupanda miti kwa idadi utakayoelekezwa na mamlaka.
3-kama utataka ujenge na uzio kwa baadaye,napo utahitaji kibali chenye masharti kama kutoinyanyua sana upande wa mbele wa hiyo "fence" kama utakavyoelekezwa na mamlaka.
4-Acha nafasi kati ya kiwanja cha majirani zako na kwako kwa vipimo utakavyoelekezwa.Usiunganishe majengo/fences kama treni ya kwenda Manyovu kule Kigoma.
5-Ukidharau kupata kibali tajwa jiandae kuvaa tisheti iliyoandikwa mgongoni "UTAJUA HUJUI"!
 
Migogoro mingi ya ardhi inasababishwa na watendaji wasio waaminifu na wenye tamaa ya pesa za rushwa. Kiukweli Tanzania kupata hati bado ni changamoto sana. Especially maeneo ya mjini.

Niliwahi kufuatilia hati ya kiwanja pale ardhi kivukoni, aiseee ndo nilielewa utendaji wa serikali kwenye nchi yetu. Duh! Sina hamu kabisa.
 
Moja kwa moja kwenye mada, Nauliza ni lazima upate kibali cha ujenzi ndipo uanze kujenga ? Na hiko kibali kinapatikana wapi, Gharama yake kiasi gani, umuhimu wa hiko kibali,

Naomba maelekezo zaidi jamani mliowahi kujenga .
Vibali ni miradi ya serikali za mitaa
 
Moja kwa moja kwenye mada, Nauliza ni lazima upate kibali cha ujenzi ndipo uanze kujenga ? Na hiko kibali kinapatikana wapi, Gharama yake kiasi gani, umuhimu wa hiko kibali,

Naomba maelekezo zaidi jamani mliowahi kujenga .
Nenda Ofisi za Manispaa uliyopo anzia Ofisi ya Mipango miji na Ardhi watakupa Utaratibu.
Ila uwe na Original 1 na Copy tatu za michoro ya nyumba yenye Mhuri wa Archtect na Kama ni ghorofa iwe na Mhuri wa Engineer.

All the best ila wengi watumishi wanapenda sana Rushwa kuwa makini
 
Hutaki wapate za kubrashia viatu na kutolea vumbi kwenye makoo yao?
 
Back
Top Bottom