Ni lazima tugawanyike; Lazima tusiwe na umoja! -Yes I said it


Je amani na utulivu utakuja wakati mwenzio ana Bilioni 1.3 katika account wewe huna hata 200 katika account?. Je umoja utakuwapo wakati kipato cha aliyenacho na asiyenacho kipo katika kiwango cha kutisha!!! Je umoja utakuwapo wakati the society is a lawless society. Je amani na utulivu itakuwapo wakati serikali ni unjust na haki anapewa yule asiyedeserve.

Marekani tunayoiimba sasa hivi haikuja hivi hivi bali ilipitia misukosuko na mitikiso mikubwa. St Augustine aliwahi sema kuwa an unjust law is similar to no law. That is why unakuta watu ni mafisadi but wanaitwa watukufu na waadilifu wengine wanawaita hata wanaume wa shoka!!!! Kimsingi nakubaliana na MM but swali langu je tufanye nini ili haki ipatikane. Serikali ishukuru mmungu watanzania ni waoga (mabingwa wa kusema tu) ingelikuwa Kenya au Uganda ingelikuwa stori nyengine. But waswahili wana msemo wao kuwa mwenye njaa hugeuka kuwa mnyama wakati fulani. Kimsingi mabadilko ya chama mbadala yanatakikana maana CCM si chama cha wanyonge tena!!!!
 
 
Watu wenye upeo tofauti kamwe hawawezi kuungana kiupeo. Ukiona watu wanadai kutogawanyika jua pana kitu aidha ni mbumbumbu wa mabao wao waoga.

Huu 'umoja wetu' amani sijui na usalama naturally haupo ni theoretical tu sema kwa vile tulipumbazwa tusiwaze tofauti na wakubwa wetu ndio tuko hapa.

Yule Mnaku alijaribu kumuelimisha mkubwa leo hana kazi.....
 
 
I take it Mwanakijiji is not pulling our collective - wink wink- legs with one of his inwardly bent but outwardly provocative satirical irony pieces.

I beg the floor to let me talk of this from the perspective of political parties as an excellent example personifying this dilemma.

Mimi nimekuwa nikilisema hili kila mara nikisikia watu wanataka wapinzani waungane ili waitoe CCM.

My point is purely on principle. Kwamba, mkiungana ili kuitoa CCM hamjaungana kikweli.Inawezekana kiitikadi hampatani.Then mkishaitoa CCM kutakuja kuwa na chaos tu. Na kuna uwezekano mkubwa wa mtu ku "pull a Kibaki".

Kwa hiyo kuungana ili kuitoa CCM basically ni kuungana ili kushinda elections. And as important as elections are, they are a means to an end, not an end in themselves (Unless you are a Jakaya Kikwete, who is brilliant at winning elections and nothing else).

Kwa hiyo I would rather see a multitude of opposition parties evolve organically, and one or two of them emerge as real challengers, than see a shotgun marriage for the intent of wining elections.The latter is sure to backfire.

Come to think of it, our opposition leaders have enough problems within their individual parties already, without even the need for a coalition to murky things up a bit more.
 

Unacho-advocate mgawanyiko ni dhana potofu kupita zote

Kinachotakiwa si kuwanyika bali ni kukubaliana katika kutofautiana

Wakati wamerakni wamekubaliana kutofautiana wamepambana kwa hoja aliyeshinda kapewa heshima yake bila maandamano na vurugu

Iran wamegawanyika matokeo yake aliyeshindwa hataki kumheshimu mshindi anapambana na mshindi kwa vurugu (aibu) tena aibu kubwa wamerakni wanamsifu aliyeshindwa (hypocracy)

ku-advocate mgawanyiko ni ku-advocate vurugu kwa nchi kama yetu

Naendelea kuamini theory yangu kwamba wewe ni msanii (playing with peoples minds)

Kutofautiana kimawazo si kugawanyika hata siku moja, tunatakiwa kuwaheshimu tunaotofautiana nao kimawazo ndani na nje ya chama na system ya serikali period!
 

Kwa hali ilivyo sasa.I strongly agree the motion.Ni bora CCM igawanyike ili mambo yaende,vinginevyo mabao yatakuwa shwari kama yalivyokuwa kwa siku za hivi karibuni kwenye ripoti ya Richmond na miswada ya uchaguzi.
 
Binafsi naona tulishagawanywa,let alone kugawanyika,mara tu baada ya kupata uhuru.Kuna tabaka lililoependelewa-aidha kama "malipo ya fadhila walizotoa kwa TANU" au nafasi walizopata baada ya uhuru wetu.Katika kundi la kwanza ni the likes of Skyes,Mwapachu,Rupia,nk.Pengine walistahili,pengine walipendelewa.Truth remains kuwa walishatengwa nasi tanguia enzi hizo.Kundi la pili ni watu ambao aidha walikuwa wajanja zaidi ya Nyerere na CCM yake,au ni matunda ya kubebana yaliyoendelea kudumu hadi sasa.Kuna akina Sir Kahama,Mungai,Kingunge na wengineo wengi ambao kudumu kwao kwenye tabaka tawala si matokeo ya ufanisi wao katika kazi bali "uteule" wao.Na kundi hili limesambaza virusi vinavyoendelea kutapakaa (angalia vigogo wanavyojitahidi kusambaza vizazi vyao katika uongozi...akina Ridhiwani Kikwete,January Makamba,nk nk).Na majuzi wameamua kuwa hilo lianze kwenye ngazi ya chipukizi (rejea uchaguzi wa chipukizi Morogoro).

Tumetenganishwa katika makundi ya waliozaliwa kutawala (wateule wachache) na sie wa kutawaliwa milele.Na sasa kwa vile siasa ni fedha,basi hiyo imegeuka fani ya wenye uwezo wa kuhonga pekee.Angalia shule wanazosomesgha watoto wao.Angalia magari wanayoendesha.Angalia sehemu wanazokwenda kustarehe.

Tulishangawanywa zamani
 

Semantics and sugar coating. Not good for your health.

Kwani kugawanyika ni lazima kuambatane na vurugu?
 
Du! Kweli mwanakijiji mpiganaji, haya tunawatakia kila la kheri, mimi nimekata tamaa,,,
 
sasa kama tafsiri ya kugawanyika ndio hizi zinazotolewa hapa , mnataka tugawanyike mara ya pili? mbona tulishagawanyika tangu zamani sana? na maendeleo ndio kama hivyo tena? huko zanzibar, no comment, subiri baada ya uchaguzi, hesabu zilizopo zinaonyesha cuf wanazidi kudidimia, subirini mtaona...............
 
Semantics and sugar coating. Not good for your health.

Kwani kugawanyika ni lazima kuambatane na vurugu?

Ndiyo kugawanyika ni vurugu lakini kukubaliana kutofautiana na kuheshimiana kutokukubaliana

Ku-advocate kugawanyika ni upotofu wa fikra na kuandaa jamii kufanya vurugu
 
Ndiyo kugawanyika ni vurugu lakini kukubaliana kutofautiana na kuheshimiana kutokukubaliana

Ku-advocate kugawanyika ni upotofu wa fikra na kuandaa jamii kufanya vurugu

Kukubaliana kutofautiana is a sorry oxymoron.
 
Kuna tofauti kati ya kugawanyika na kutofautiana. Tunatofautiana. Hatujagawanyika. Wala hatutagawanyika kamwe. Umoja na mshikamano ni urithi wa Chama kilichotukomboa.Tuuenzi na kuulinda umoja na utulivu. Kwa pamoja, Mwanakijiji, Mwanajiji, Mkulima, Mfanyakazi, Mfanyabiashara na Mwekezaji, tujenge Taifa letu changa.

Umoja ni Nguvu!
 

Exactly!

Kutofautiana kwa mapato, mawazo, elimu, dini si kugawanyika hiyo ndio hazina ya maendeleo katika jamii..kwani sisi si kondoo!

Kugawanyika ni upotofu wa fikra na dalili za kukata tamaa kihoja

Si tabia njema ku-advocate kugawanyika badala yake tunatakiwa ku-advocate kutofautiana katika mambo na kuwa pamoja katika kuheshima mawazo ya wengi na wachache ata the time!
 

Naam umenena. Binadamu wote ni sawa. Walalaheri kwa Walalahoi. Wamachinga kwa Wawekezaji. Sote ni ndugu.
 

Watu wanaweza kuwa pamoja wakati wakitofautiana lakini wakagawanyika wakati wa kufanya maamuzi yanayosababishwa na kutofautiana huko.....Msisitizo kwenye "Maamuzi"
 
kuna kila dalli kuwa hapa jamvini kuna watu wana kazi ya kumpigia makofi mwanakijiji hata kama hawajaelewa ametoa mawazo gani!!!!!!!!!!!

jamani jaribuni kuthink critically, kama ni kutofautiana kimtazamo, matakwa, itikadi nk. mbona tayari tunatofautiana? tutofautiane mara mbili? au mara ngapi???

ishu ni "kugawanyika" nipeni mfano wa nchi kama yetu hususani ya kiafrika "iliyogawanyika" halafu hapakutokea mapigano/umwagaji damu na badala yake waka[pata maendeleo..............

nakubaliana na hoja za tumaini na companero..............
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…