Ni lini JWTZ watatoa majina ya kuitwa kwenye usaili?

Sikupingi ila hii ya kusema uanze kupasha ili ukifika kule uwe umezoea unajidanganya..hio siku ya kutolewa uraia ikianza ndio utajua kwanini ata mungu siku ya saba alipumzika
Mwambie kabisa ajue kozi haitaji maandalizi watu wanapiga push up mkapa unalia up kushoto
 
Kunjua moyo unatoboa haufi kama afya ipo vizuri unamaliza
Nakumbuka niliwahi kuwa Skaut shule ya msingi, sasa kuna kipindi tukatangaziwa kwenda kambi wiki nzima, nikamwambia mshua akasema nenda akanipa na pesa ya mchango 2500/=, kumwambia bimkubwa akakaza hamna kwenda, na mie nilikua napenda kweli mambo za skauti tulikua tushapewa skafu za kuvaa shingoni hapo nafukuzia kupata gwanda la kaki,na bellet na kupata gwanda lazima uhitimu mafunzo.

Nikasema usinitanie wewe, nikatoroka hom, na kibegi kina,sahani, kikombe, kijiko, boxer mbili, Mswaki, dawa ya meno, pensi na sweta. Kufika kambini ilikua jioni, tukaimba chenja za kutosha, tukala ubwabwa halafu tukalala madarasani, maana kambi ilikua kwenye eneo la shule . Kesho yake asubuhi wakatakiwa watu kumi wakalete kuni na mie nikachaguliwa miongoni mwao. Tukaondoka kuleta kuni saa 12 alfajiri, mwendo mrefu kidogo.

Kurudi Jua limeshachomoza ilikua mida ya saa nne asubuhi Kamishna akasema tumefanya uzembe, na adhabu kali itatolewa kama fundisho kwa wengine. tukapewa adhabu ya kukimbia kuzunguka bendera ya ile shule nonstop, kamishna akaingia zake ofisini.Tukaanza adhabu chap.Tulikimbia kuzunguka ile bendera tukaloa jasho na vumbi la kutosha miguuni,Hatukula asubuhi wala mchana kila mmoja anasonya tu. Kuna jamaa mmoja alikua muoga kweli akawa anatukataza kusonya anasema Kamishna akisikia tutaongezewa adhabu. kamishna anakuja kutoka saa nane mchana anakuta bado tunakimbia kuzunguka ile bendera Jamaa anajifanya kutushangaa eti " Ah bado mnakimbia tu, niliwasahau aisee haya nendeni mkale " Tukaitikia asante mkuu, wakati tunajua fika watu washakula cha mchana hivo ni kusubiri cha usiku, mda huo nishaanza kumkumbuka maza alivokua ananikataza kwenda kambini.

Mpaka hapo nikawa nishaingiwa kinyongo na Uskauti wenyewe, nikajisemea ikitokea kazi nyingine naenda halafu natoroka, maana mazingira pale kambini yalikua hayaridhishi, vyoo vya shule matundu machache, hakuna maji,kulala kwenye madawati ama ukikosa unalala chini, maana tulikua wanafunzi shazi. mbu nao wakutosha.Haikuisha hata siku jioni ya siku ileile nikasikia wanahitajika vijana wa kwenda kuchota maji, nikasema fursa ndo hii sasa ya kuondoka Guantanamo.

Nikaenda chap tukahesabiwa watu 20, Tukapewa ndoo za lita kumikumi kila mmoja na yake, nikaanza kuwaza kuhusu kibegi changu, niko nacho mgongoni saa hiyo, natokaje nacho getini sasa. na getini kuna skauti wanoko hatari yaani wanajikuta makomando mixer kutembea juu ya kamba na kuruka moto. nikasema sio kesi Tulivokaribia getini nikamshtua jamaa mmoja ambaye tulikua pamoja kwenda kuchota maji, nikamuomba anishikie ndoo yangu ili nikaweke begi halafu nakuja. na wale maskauti wa getini wakaona tunavokabidhiana ndoo, na nilifanya makusudi ili nitakaporudi wazinizuie kutoka nje.


So nikampa jamaa ndoo yangu halafu nikakimbia kwenye darasa tuliokua tunalala nikaingia nikaenda mpaka kwenye madirisha ya upande wa nyuma nikalidondosha begi kwa nje halafu nikarudi mbio kuwahi getini, kufika pale nikakuta wenzangu washatoka nje, kwakua wale maskauti walishaniona nilivokua nakabidhi ndoo kwa mwenzangu hawakunitilia shaka wakaniruhusu nitoke. nilivotoka nje mzeeee. nilikula kona chaap, mpaka nyuma ya ile shule nikaokota kibegi changu halafu nikala kona kwenda hom.


Kufika Hom jioni ileile nakuta maza kakaa nje anachambua mchele namuamkia haitikii. ananiangalia miguuni nilivopauka, nikajua leo lazima kiwake usiku dingi akirudi. nikaingia chumbani kwangu nikajifungia humo, usiku mshua karudi nikaitwa mezani maza anasoma mashtaka anadai nitafute pa kwenda kuishi, kijana wa darasa la tano naenda kuishi wapi sasa. nikaomba msamaha pale na Nikawasimulia kilichonikuta, Maza alinicheka kinoma, so kambi ya wiki nililala usiku mmoja tu. Sijui huko rts itakuaje.​
 
Naona utatoroka wiki ya kutolewa urai wewe kule zoezi jepesi ni push up tu kuna mapenzi ya nyoka kutundika ni zoezi nalichukia zaidi na adhabu ya batakanya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…