Ni lini mchezo wa ndondi (boxing) utaboreshwa? Habari ya vifo vya mabondia zinaumiza

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Habarini wakuu!
Mimi nimekuwa si mnazi sana wa mchezo wa ndondi; nimejikita zaidi katika kufuatilia mchezo wa soka. Aidha, katika kufuatilia soka katika kurasa mbalimbali za michezo nimekuwa nikikutana na habari za mabondia kufariki ulingoni mara kwa mara.

Zaidi ya hilo, kupitia kurasa mbalimbali za michezo wanaweka bayana kuwa katika kipindi cha miezi sita ndani ya mwaka huu (2019), kuna mabondia sita ambao tayari wamefariki ulingoni kutokana na kupata majeraha kichwani (yaliyosababisha damu kuingia kwenye ubongo). Kimsingi, binafsi nimekuwa sifurahishwi na habari hii na naona kuwa jambo hili lina athari kubwa kwani linaweza kuwakatisha tamaa watu wenye ndoto za kuwa mabondia nguli baadaye.

Hivyo, kutokana na hali hiyo kukithiri, ni jambo gani tunafikiri Shirikisho la Ndondi Duniani (W.B.O) linapaswa kufanya ili kulinda usalama wa mabondia dhidi ya madhara hayo?
Naombeni mchango wenu wadau.
 
Kiimani unalizungumziaje hili swala?

( وَأَنفِقُوا فِي سَبِيلِ اللَّهِ وَلَا تُلْقُوا بِأَيْدِيكُمْ إِلَى التَّهْلُكَةِ ۛ وَأَحْسِنُوا ۛ إِنَّ اللَّهَ يُحِبُّ الْمُحْسِنِينَ )

البقرة (195) Al-Baqara

Na toeni katika njia ya Mwenyezi Mungu, wala msijitie kwa mikono yenu katika maangamizo. Na fanyeni wema. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao wema.
 
Unajua kila mchezo una risks zake. We mtu unaingia ulingoni, unatutuswa kichwa tu kwa masaa, unategemea kutakuwa na uzima hapo? Ndo' mana hawa wacheza boxing hata wakija staafu vichwa vyao huwa havipo sawa. Nakumbuka kuna siku Cheka, kama sijakosea, alisema amekuwa mtu wa kusahau sahau sana kiasi kwamba anapoteza simu zake mara kwa mara.

Kama kuna namna ya kufanya kwenye hayo, ni wazi tena hakutakuwa na namna ya kufanya boxing iwe na mvuto wake qa siku zote au kama ilivyozoeleka.
 
Takwimu zinasema tayari zaidi ya mabondia 500 wamekufa ulingoni.

Kwa Africa, South Africa wanaongoza kwa mabondia wao kufariki huku wakipigana
 
Niliwahi pia kumuona Mohamed Ali akisumbuliwa na ugonjwa wa kutetemeka,sijui kitaalamu unaitwaje.Ila watu walidai ni matokeo ya mchezo wa boxing
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…