Ni lini Tanzania itawapa nafasi kushika nafasi ya...

Ni lini Tanzania itawapa nafasi kushika nafasi ya...

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
...urais vijana wa Tanzania?

Tunaona wenzetu Wamarekani pamoja na kuwa ni Taifa kubwa lakini limewaamini vijana wenye umri sawa na miaka ya uhuru wa Tanzania. Obama ana miaka 47 na VP wa Mcsame ana miaka 44.

Rais anayefuata wa Tanzania 2010, kwa maoni yangu, asizidi miaka 45. Swala la kutokuwa na experience halipo maana hao wenye experience kama fisadi Mkapa tunajua alifanya nini alipokuwa madarakani na JK ambaye naye ana 'experience' nchi imeshamshinda siku nyingi anachokifanya sasa hivi ni kujibaraguza tu.
Waungwana mnasemaje?
 
Mzee wangu,

Nadhani umesahau kuwa tulianzia huko huko ila wale waliotutangulia wakaamua kuwa wachoyo wa madaraka na kuwatupia vijana nje nje, kwanza kwa kuweka Azimio la Musoma, halafu baadey wakaleta vikwazo vya hapa na pale. Nyerere alianza kuongoza nchi hii akiwa na umri wa miaka 39 tu, na vile vile alianza kuongoza chama chake cha TANU akiwa na umri wa miaka 32 tu. Ndiyo maana ukiona picha za kwanza za Nyerere akiwa Ikulu, zinaonyesha sura ya kitoto kabisa, kwa mfano hii hapa

attachment.php
 
Ni kweli Kichuguu tulianzia huko lakini sasa hivi tumeng'ang'ana na vizee tu kwa kisingizio cha uzoefu. Hata ukipitia majina yanayosemwa kumrithi JK 2010 au 2015 wengi ni waliokula chumvi nyingi. Kuna haja ya kuwapa vijana nafasi ya kuja na mawazo mapya badala ya hawa wazee ambao wametuangusha katika kila chaguzi with exception ya Mwalimu.
 
Ni kweli; katika sehemu nyingi duniani hapa, viongozi vijana wamesaidia sana nchi zao kuliko viongozi wazee. Angalia enzi za Clintoni huko Marekani, wakati huo alikuwa kwenye 40's tu. Kumbuka miaka ya sitini jinsi Nyerere alivyofanya mageuzi sana Tanzania akiwa kwenye 40's tu, Sokoine alifanya mengi lakini akiwa kwenye 40's tu. hata kule Zimbabwe, Mugabe alikuwa shujaa sana kabla hajavuka ikweta. Nafikiri njia ya kwanza katika kutatua jambo hili ni kuweka term limits kwenye nafasi zote za kisiasa.
 
Ni kweli Kichuguu tulianzia huko lakini sasa hivi tumeng'ang'ana na vizee tu kwa kisingizio cha uzoefu. Hata ukipitia majina yanayosemwa kumrithi JK 2010 au 2015 wengi ni waliokula chumvi nyingi. Kuna haja ya kuwapa vijana nafasi ya kuja na mawazo mapya badala ya hawa wazee ambao wametuangusha katika kila chaguzi with exception ya Mwalimu.

sawa sawa naunga mkuno kuwa wapewe vijana nchi kwani hawa wazee na sera zao ni za zamani na ndio maana rais anasema kuwa vumilia shida badala ya kutafuta mbinu ya kufanya maisha bora kwa maana nyingine kuwa sera zao ni kuwa haiwezekani inabidi tuendelee kuishi hivi hivi
 
Suala kubwa ni kujitokeza nakuhimili mbinde,vishindo, makeke,mikwala na mizengwe ndani ya chama chako mpaka ushindi upatikane.
Huyo jamaa wa kuhimili mikiki hiyo ni nani??
Huyo jamaa wa kujitokeza kuhimiri vishindo si mwingine ni wewe na mimi.

Obama amesema mabadiriko hajaji kutoka Ikulu ila yanakwenda Ikulu yakitokea mtaani.
 
Back
Top Bottom