Ni lini tutaacha Kumsimanga Hayati Magufuli na kumuonesha kuwa hakuwa Rais mpenda Watanzania?

Wanamsimanga sana MAGU Halafu kwa mambo ya kipumbavu pumbavu tu...
 
sifa za watz πŸ˜€πŸ˜€

kuna mtu alisifiwa kama Magufuli akiwa hai?
nyimbo na tunzi tuliimba sana kumsifia.

So usijali ni utamaduni wetu tu, si umeona asubuhi kwaya zilivyopamba kwa mashairi, ni nyimbo tu, by the way people are not seriousπŸ˜‰πŸ˜‰
 
Kinachonishangaza kuna Mtu ndiyo alikuwa Msaidizi wake na hata 85% ya Maamuzi nae alihusika ila leo Magufuli hayuko tena nasi duniani amejitoa na sasa Kinafiki / Kiunafiki anataka Kuwadaa Watanzania Kuonyesha kuwa Yeye hakuwa Mtu mbaya.
Hivi Kwa akili ya kawaida tuu unadhani magufuli alikuwa akimshirikisha msaidizi wake mambo yake!?? Hebu shirikisha ubongo kidogo tuu!!!
Nakupa mfano mdogo Sana, Kumbuka wakati wa kumteua katibu kiongozi baada ya yule wa Mwanzo kufa unadhalini akimshirikisha msaidizi wake!?
 
Wanaolipwa humu JF Kumsimanga JPM,Siku wakiacha kulipwa masimango yataisha.

Hao wengine,ukifika uchaguzi ndiyo watajua ,kuwa walikosea Kumsimanga JPM.

Ujue wapiga kura JPM,walimuelewa sana
 
Habari za kuamka Mkuu,
Naungana na wewe kupinga Rais wa Sasa ambaye alikuwa msaidizi Mkuu wa Magufuli anapomnanga Kwa dhuluma mbalimbali alizowafanyia baadhi ya Watanzania. Lakini kama waliodhulumiwa wakisema wenyewe ni haki yao acha waseme. Magufuli kama ulivyosema naye kama binadamu alikuwa na madhaifu kama Mimi na wewe lakini ukweli usemwe alikuwa na madhaifu Makubwa wala si madogo kama wengine wanavyojaribu Kutuaminisha. Annual Increment iliyosemwa Jana ni haki iliyo kwenye mkataba wa kazi. Yaani ni kipengele katika Katiba ya Utumishi, lakini Kwa makusudi tu Katiba hiyo ilikanyagwa Kwa tamko la Mtu mmoja ambaye ya kwake haikupunguzwa hata senti. Bora hata ingekuwa hela kubwa basi, kinachoongelewa ni hela ndogo kiaasi kwamba kuna Watumishi Annual Increment ni 4,000 tu. Watu wamefanya kazi Miaka 6 hakuna kilichoonhezeka kwenye mshahara huku maisha yakiendelea kupanda. Tuwe wawazi, Magufuli aliwaonea Watumishi.
 
Miaka 6 bila nyongeza ya mishahara kila mwaka kama takwa la kisheria kwanza inabidi watumishi wadai malimbikizo ya miaka hiyo 6 ikibidi mali zake ziuzwe
 
Tutaacha siku tukimuona Ben Saa nane akiwa hai.
 
Ungejua hiyo increment inayozungumziwa ni kiasi gani wala usingehangaisha kichwa chako,na ipo kisheria ila mwendazake aliamua kuikanyaga kama alivyokanyaga sheria nyingi tu,..kashaenda yaliyobaki yanafanyika yanafanywa na walio hai nao watajiondokea acha stress mzee
 
Kinachonishangaza kuna Mtu ndiyo alikuwa Msaidizi wake na hata 85% ya Maamuzi nae alihusika ila leo Magufuli hayuko tena nasi duniani amejitoa na sasa Kinafiki / Kiunafiki anataka Kuwadaa Watanzania Kuonyesha kuwa Yeye hakuwa Mtu mbaya.
Siku zote msaidizi anakubakiana na bosi wake kinafiki. Hata kama anajua analoamua bosi ni baya maana akibisha tu uteuzi unayeyuka. Hata Khrushev alikuwa msaidizi mwaninifu wa Stalin alipoimbia madarakani alimkosoa Stalin.
Kwa hiyo sii ajabu kabisa maamuzi ya mtangulizi yakabadilishwa anapoongia msaidizi. Ndio yanapotokea Kwang'a Uhuru na Ruto.
 
huo mshahara wa kila mwezi unaongezwa hapo nyumbania kwenu? hivi we unamfahamu hata mamako aliyekuzaa kwa huo upumbavu ulionao?
 
chema chajiuza kibaya chajitembeza. Msiwalazimishe watanzania kukumbuka mateso waliyoyasahau. Yule alikuwa shetani hakuna anayemkumbuka msitulazimishe we kenge. km unampenda sana mfuate aliko au hujui njia ya kufika kwake tukuelekeze we nyau?
 
Magufuli anatembea na historia ya aliyoacha duniani!
Ukiacha wema utakumbukwa kwa wema, ukiacha ushetani utakumbukwa kwa ushetani!
Tuache matendo yajiuze na sio kulazimisha tofauti na matendo yake!
 
Punguza makasiriko ndugu !!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…