Ni Lini Wizara ya Elimu itatoa majibu?

Ni Lini Wizara ya Elimu itatoa majibu?

Tiba

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2008
Posts
4,605
Reaction score
3,176
Wana Jamvi, Ni karibu miezi miwili imepita sasa tangia matokeo ya mtihani wa darasa la saba yalipotolewa. Hivi tunakaribia kuingia January lakini Wizara ya Elimu bado haijawapangia shule wanafunzi waliofaulu mtihani huo. Kuna mtu anajua ni lini tutarajie hayo majibu? Hivi tarehe za vijana wa kidatocha kwanza kuanza masomo umebadirika siku hizi?

Tiba
 
Imeshatoa majibu. Alitangaza Katibu Mkuu - TAMISEMI. Fuatilia mada, hata huku Jukwaani.
 
Jamani ina maana hakuna anayejua wizara inasubiri nini kutoa majibu ya vijana waliomaliza darasa la saba mwaka huu na kufaulu mtihani ni lini watapangiwa sekondari? Kwa kufahamu kwangu mpaka sasa haya majina ya nani kapangwa shule gani yanapashwa kuwa yametoka kwani January ndio hiyo iko karibu kabisa.

Anayejua kinachoendelea atujuvye tafadhali.

Tiba
 
Imeshatoa majibu. Alitangaza Katibu Mkuu - TAMISEMI. Fuatilia mada, hata huku Jukwaani.

Ningependa kuona hiyo list ya nani kapangwa shule gani. Wapi ninaweza kuona hiyo kitu. Kwa nini list ya mwanafunzi yupi kapangwa shule gani itolewe na katibu mkuu TAMISEMI na wala sio Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu?

Tiba
 
Back
Top Bottom