Abdul Najad Faiq
Member
- Jul 13, 2021
- 7
- 5
Na:Abdull Najad Faiq
Unapo zungumzia Tanzania huwa ina maana 2 tofauti kulingana na katiba ya Jamhuri Tanzania ni jina lililopatikana baada ya kuungana kwa nchi ya Tanganyika na nchi ya Zanzibar ambapo ulizaliwa umoja wa "Jamhuri ya Muungano ya Tanzania" lakini baada ya muungano ule jina la Tanganyika likafa ghafla,badala yake likasimama jina jipya la Tanzania
Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema " Eneo la Jamhuri ya Muungano ni eneo lote la Tanzania bara na Tanzania Zanzibar".
Pia katiba haikuishia hapo ikaendelea kwa kusema"Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaweza kuigawa Zanzibar katika wilaya na mikoa kwa kushauriana kwanza na Rais wa Zanzibar.
Ukiisoma katiba ya Zanzibar inasema kwamba" Zanzibar ni miongoni mwa nchi 2 huru zinazo unda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Pia ikaendelea kwa kusema"Eneo la mipaka ya Zanzibar ni pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba,eneo lote la bahari pamoja na visiwa vidogo vidogo vinavyo izunguka".Ikandelea tena"Rais wa Zanzibar ataweza kuigawa Zanzibar katika Mikoa pamoja na Wilaya.
Kwahiyo ukiziangalia katiba hizi 2 utaona migongano,Zanzibar haijawahi kusalimisha mamlaka yake kwa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,hata jina la "Tanzania Zanzibar" Baraza la Wawakilishi hadi leo halija liafiki jina hili wala kulipitisha ndani ya katiba yao na hii inampa nguvu Rais wa Zanzibar juu ya jambo lolote linalo ihusu Zanzibar hata kama katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inachukuliwa kuwa ndio katiba mama kwa pande zote 2 za Jamhuri ya Muungano
Ukija katika orodha ya mambo ya Muungano,katiba imetoa mwanya kwa kila mshirika kujitegemea kwa mambo yote yasiyo ya Muungano ambapo Tanganyika bado itaendelea kuwakilishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ila Zanzibar itajisimamia yenyewe
Kiuhalisia Zanzibar na Tanzania sio nchi moja ila kuna mambo nyeti tuna share ambayo yanatufanya tuonekane tuwamoja ila kila sehem ina mipango na maslahi yake tofauti,ndiomaana sheria na bajeti za Zanzibar hutungwa na hupitishwa katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar
Mfano mwengine Bunge la Tanzania ambalo limebeba sura ya Muungano linatoa nafasi kwa Wabunge wa Zanzibar kushiriki sababu kuna Wizara kama Mambo ya ndani,Mambo ya Nje,Fedha,Ulinzi,Mawasiliano,Mazingira zote hizi tuna share ila linapokuja mathalan jambo la ujenzi wa miundombinu ya nchi pamoja na uwekezaji huwa hatushei pamoja kwahiyo Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania halipangi wala kupitisha bajet juu ya ujenzi wa miundombinu yoyote kwa Zanzibar,kuvutia uwekezaji wala kujenga miradi ya maendeleo ya kimkakati,mfumo wa namna hii hatuwezi kusema kuwa sisi ni wamoja sababu ujenzi wa miundombinu ni katika jambo la kipaumbele zaidi linalo onesha kwamba nyinyi ni wamoja
Uwepo wa timu 2 tofauti za taifa baina ya Zanzibar na Tanzania bara ni uthibitisho mwengine unao onesha kwamba sisi sio wamoja katika kila kitu,kinacho wafanya wachezaji wa Zanzibar kushiriki katika timu ya taifa ya Tanzania ni kutokana na kule Zanzibar kukosa uanachama wa CAF na FIFA hivyo haina uwezo wa kushiriki mashindano yoyote ya kimataifa,
Michezo sio jambo lililo katika orodha ya mambo ya muungano ila Zanzibar imekua ngumu kupata uwakilishi kimataifa sababu Wizara ya Mambo ya Nje tunashea pamoja baina ya Zanzibar na Tanganyika ila Tanganyika inanufaika sababu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jicho jengine ndiyo hiyo hiyo Serikali ya Tanganyika
Muundo wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haufanani na muundo wa Marekani ila unafanana katika suala la mantiki yake,nafikiri walio unda muundo wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hawakua direct kutokana na kwamba Zanzibar ilitoka katika Mapinduzi ya kumuondoa Sultan ambayo yalitazamwa kuwa ndio Uhuru kamili,ingekua ni ngumu mno kuwaambia watu waliotoka kujikomboa waungane nawe wawe nchi moja,wapoteze utaifa wao,silka pamoja na kile walichokua wakikipigania.