Ni Lissu au Mbowe?

Mingendeu

Senior Member
Joined
Aug 26, 2019
Posts
115
Reaction score
237
Kila mwenye mapenzi ya siasa za Tanzania, basi macho na masikio yake yapo CHADEMA kuelekea uchaguzi wao mkuu. Hii inaonesha ni kwa namna gani CHADEMA ni bidhaa muhimu kwenye siasa za Tanzania. Wanaosema CHADEMA ndicho chama cha upinzani chenye ushawishi mkubwa Tanzania bara, wanayo hoja. Sio wakubezwa.

Je!! Ni Lissu au Mbowe?? Ni swali lililogawa wanachama na wasio wanachama. Nguvu ya ushawishi ya Mbowe ndani ya chama inaenda kushindana na nguvu ya Lissu ya nje ya chama. Sijui nini kitatokea? Natamani kuona Mbowe anashinda ili nisikie maamuzi ya Lissu na timu yake. Lakini pia natamani kuona Lissu akishinda ili nione uimara wa Chadema bila Mbowe, pia uimara wa Lissu kwenye kuongoza taasisi kubwa hiyo.

Kuna nyakati natamani kuona Mbowe kashinda uwenyekiti, Ila umakamu ashinde Heche ambaye amejitangaza kuwa timu Lissu. Pia natamani Lissu ashinde uwenyekiti lakini Wenje ashinde umakamu. Kiufupi uchaguzi wa CHADEMA ni wa moto.

Busara za Mbowe na Lissu baada ya uchaguzi wa chama chao unaweza kuleta funzo kubwa sana kwenye historia ya siasa zetu.

Kama chama kitashikamana baada ya uchaguzi huu. Wakakubaliana kwenye matokeo, basi watakuwa wametufundisha maana halisi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo kwa vitendo.

Kila la kheri CHADEMA, kila la kheri Mbowe na Lissu. Uchaguzi wenu umebeba hatma ya upinzani wa Tanzania. Msituangushe.
 
Siasa zipo kushoto, ila natamani kumuona TL akishika usukani nione upinzani wenye sura mpya....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…