Ni lugha tu iliyosababisha Mnara wa Babeli kutojengwa?

Rangoo

Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
99
Reaction score
114
Katika mapokeo ya Mwanzo 11 Babeli ulikuwa mji wa kwanza uliojengwa baada ya gharika kuu. Binadamu waliamua kuwa na jengo kubwa katika mji na kilele chake kifike mbinguni. Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyechanganya lugha ya watu ambao hivyo walilazimika kuachana baadaye bila ya kukamilisha mnara wao.

Sasa Swali langu hapa Linakuja Kwa Wachambuzi wa Mambo . Je! Ni lugha pekee au Mungu aliwapiga Kitu kingine maana Wangeweza Hata Kutumia Lugha ya Picha Na Ishara kuendelea Kuujenga Mnara

Je kitu gani zaidi kilitokea mpaka Wakaamua Kuhairisha?
 
hizo ni hadithi za kale ambazo hazina ukweli wowote... huko mbinguni ni wapi walikokaribia kufika? Je hizo ndege na roketi za siku hizi hazikaribii kumfikia huyo Mungu?
 
pasipo na mawasiliano au lugha moja hapawezi kuwa na maendeleo
 
Mbingu iko wapi kila siku wana anga wanapaisha setilite lakini hawaikaribii mbingu ila wanakutana na mawingu tu
 
hizo ni hadithi za kale ambazo hazina ukweli wowote... huko mbinguni ni wapi walikokaribia kufika? Je hizo ndege na roketi za siku hizi hazikaribii kumfikia huyo Mungu?
Nakuunga mkono mkuu.
 
ngoja niketi kiti cha mbele kutafakali maswali fikilishi
 
kocha mchina, winga mjaluo, kiungo myunani, kipa mhindi, beki mwarabu na hawaongei lugha moja. mbona mwalimu anawafundisha na wote wanamwelewa
 
Mkuu pale ilikuwa sio mnara wa kupanda physically hadi mawinguni....nooo.
Walikuwa wanajenga mahali pa kukutana na miungu yao na kufanya kafara na ssdaka mabal mbali.
Mungu akaona watamwasi. Yanini kuwaacha wajenge mahali pa kumwasi?
Na tazama akavuruga kusikilizana kwao
 
nasikia hawakuwa na lengo la jufika mbinguni hasa lengo lao lilikuwa kwenda kipaza sauti kwa sir God
 
NNadhani hatujaelewa maana halisi ya ujenzi wa mnara huo, sidhan kama ni mnara uliophysically kama tunavyodhania. Kwanza mbinguni ni wapi haswa?
 
Katika mapokeo ya Mwanzo 11 Babeli ulikuwa mji wa kwanza uliojengwa baada ya gharika kuu. Binadamu waliamua kuwa na jengo kubwa katika mji na kilele chake kifike mbinguni. Mpango huu haukumpendeza Mungu aliyechanganya lugha ya watu ambao hivyo walilazimika kuachana baadaye bila ya kukamilisha mnara wao.

Sasa Swali langu hapa Linakuja Kwa Wachambuzi wa Mambo . Je! Ni lugha pekee au Mungu aliwapiga Kitu kingine maana Wangeweza Hata Kutumia Lugha ya Picha Na Ishara kuendelea Kuujenga Mnara

Je kitu gani zaidi kilitokea mpaka Wakaamua Kuhairisha?
Nafkiri upite hapa usome maoni ya wadau natumaini utapata majibu yote

Mnara wa Babeli na historia ya kutisha
 
hizo ni hadithi za kale ambazo hazina ukweli wowote... huko mbinguni ni wapi walikokaribia kufika? Je hizo ndege na roketi za siku hizi hazikaribii kumfikia huyo Mungu?
Nazani zinaenda angani sio mbinguni
 
Back
Top Bottom