Dr. Walter Rodney ktk kitabu chake ... How Europe Underdeveloped Africa ... anasema (kwa tafsiri ya kiswahili) ... Ukiona mhudumu wa Ofisi anaiba rimu ya karatasi, usijisumbue, siyo yeye; Na ukitaka kudhibiti wizi na kuimarisha maadili kazini, panda juu kwa Katibu Mkuu wa Wizara kwani huko ndiyo kuna uozo mkubwa ... Hakuna Mtumishi mwajiriwa anayeweza kufanya vizuri au vibaya isipokuwa amemwona wa juu yake (Boss) anafanya.
Inasemekana, (mie binafsi sina ushahidi kwani sijawahi pata tatizo na Takukuru) Takukuru inaongoza kwa ku-promote rushwa Nchini.
Habari ndiyo hiyo.
Ni vigumu sana kwa rushwa kukomeshwa ktk Nchi nyingi za Africa kwa sababu Taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali zipo zinastawi na kufaidika na mifumo ya rushwa. Bila rushwa haziwezi kushinda tenda, chaguzi mbalimbali n.k. Bila rushwa haziwezi kutawala watu. Bila rushwa haziwezi kufanya biashara. Ni rushwa, ni rushwa tu kila mahali.
Anyway, kitu ambacho watu wengi hatukielewi ni kuwa rushwa ni mfumo wa kiroho unaoratibiwa na kuendeshwa na shetani mwenyewe ktk ulimwengu wa roho. Takukuru, Tiss, Polisi n.k. hawawezi kamwe kukomesha rushwa. Bwana Yesu Kristo mwenyewe ndiye anaweza kukomesha rushwa kwa njia ya kuwaweka watumishi wake waadilifu ktk Taasisi hizi. Watu wenye hofu ya Mungu. Watu waliojikana na wameubeba msalaba wao. Watu wasioipenda dunia kwa sababu wanajua Wao ni wageni wapitaji tu hapa Duniani. Wanaamini kuwa utauwa na kuridhika ni faida. Wanajua kuwa hapa Duniani walikuja uchi na wataondoka wakiwa uchi. Kwao kwa milele ni mbinguni alipo Bwana Yesu. Watu wanaompinga na kumkemea shetani na wanamkataa pamoja na mambo yake yote. Wakristo wakiookoka kweli kweli.