Makyao,
Tatizo moja ni kwamba tumeingia katika mfumo wa vyama vingi bila kuelewa vyema vyama vingi vina wajibu gani kisiasa. Vyama vya siasa vimekuwa vikiwaza zaidi ni jinsi gani vinaweza kuingia kushika madaraka ya nchi bila kuzingatia maana nzima ya mfumo wa vyama vingi. Matokeo yake vimekuwa vikiona njia ya mkato ya katika kufikia azma ya kushika uongozi wa nchi ni kutumia ama kubebea bango shughuli za maendeleo na kujinadi kwamba vyama vyao vikipewa dhamana ya uongozi ndivyo vyenye uwezo wa kuleta maendeleo hayo na kusahau kwamba maendeleo yanapaswa kuletwa na wananchi wenyewe kwa utashi na muongozi wa Serikali.
Tatizo jingine ni mmomonyoko wa maadili miongoini kwa viongozi wa vyama vya siasa na hata wananchi/wanachama wa vyama hivyo kwa ujumla. Vyama vya siasa kuanza kujipigia debe kwa kuorodhesha masuala ya maendeleo ni kudhihirisha jinsi ambavyo vyama vimekuwa na watu/viongozi wasio waadilifu ambao wamekuwa tayari kusema uongo na ulaghai mwingi ili wafanikiwe kupata wanachotaka.
Ujenzi wa barabara,
Ujenzi wa shule,
Ujenzi wa vituo vya afya,
Kuanzishwa kwa SACCOS,
Ujenzi wa viwanda vidogo,
n.k
ni kazi na shughuli za maendeleo ambazo zinapaswa kufanywa na Serikali ikishirikiana na wananchi kwa ujumla na si jukumu la chama ama vyama vya siasa. Zipo Serikali za kijeshi ambazo mapinduzi yake yaliweza kufanywa kwa manufaa ya umma. Serikali hizo zimeweza kuendeleza shughuli za maendeleo ya nchi bila kuwepo siasa ya aina yoyote ndani yake na bila kuwepo vyama vya siasa. Kwa maana hiyo basi hakuna sababu yoyote ya msingi ya kutaka kuhusisha propaganda za chama fulani katika kutafuta ama kuleta maendeleo nchini. Maendeleo hayaletwi na siasa/propaganda za vyama bali huletwa na juhudi za Serikali iliyo madarakani ikishirikisha wananchi kwa ujumla.