Ni maeneo gani ya kujiajiri?

Ni maeneo gani ya kujiajiri?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,136
Reaction score
32,268
Hello JF,

Kwanza poleni na msiba(may he RIP)

Leo ningependa kujua apart from kilimo ambacho huwa mnasema humu,Je ni maeneo gani mengine ambayo mtu anaweza kujiajiri?

Hii itatoa mwanga sio tu kwa watu wanaohangaika na ajira,

bali hata wanaounda mfumo wetu wa elimu,iwe kama pointer masomo gani yatiliwe mkazo,

haya karibuni

Becky
 
Meneo ya kujiajiri hutegemea na uwezo wa mhusika pamoja na fursa ya eneo lenyewe.

Unaweza kuuza samaki kijiji cha wamaasai?
 
jamani tajeni zote zilizopo Tanzania mtakua mmewasaidia wengi,haya taja fursa ziliopo umasaini?
Dada yangu, biashara ni zilezile tu kama unavyoziona sema tu unaweza kuzifanya katika njia iliyoboreshwa zaidi.

Kuna dada mmoja ninasikia anauza makande lakini kwa njia ya kisasa zaidi na sahani moja ni karibia 5,000/=

Wewe pia unaweza kuwa mama lishe kwa njia ya kisasa zaidi. Hakuna jipya chini ya jua.
 
Basi graduates wakilalamika huku hamna ajira msisiseme hakuna ajira kajiajiri bila kutaja nini specific afanye, kundi kubwa la wasio kwenye ajira sidhani kama ni wote hawajui mazingira yao, kwa nyie wazoefu ndio mtushike mkono sisi wengine
 
Unaweza kujiajiri kwenye kitu ulichonataaluma au ujuzi nacho, ikiwa huna ujuzi waweza kujifunza.

1. Upishi na uuzaji wa vyakula, hii nadhani inaongoza kwa kujiajiri kwa wote wanawake kuanzia mama/baba ntilie mpaka kwenye migahawa, catering. Mtaji wake pia sio mkubwa kutegemea na level yako.

2. Ufundi
A. Ujuzi wa ufundi seremala kutengeneza fenicha mbali mbali umeajiri vijana wengi sana hasa wale wenye ubnifu wanaotumia mitandao ya kijamaa kupata wateja wengi mpaka wanageuka matepeli wanachukua pesa wanashindwa kutoa bidhaa. Hii ni kujifunza veta na kuwa mbunifu tu, vijana wengi wamjiajiri na ina walipa.

B. Ufundi magari, umeme, ujenzi, bomba, tiles, rangi n.k. hizi ni kati ya njia za kujiajiri zinazolipa muhimu uwe na ujuzi na uzoefu na kazi zisizo za kubabaisha.

C. Tailor

3. Fursa katika burudani na Ushereheshaji

Tasnia ya sherehe, harusi na burudani inatoa fursa nyingi za kujiajiri kama ifuatavyo, kanuni ya kufanikiwa ni rahisi fanya kazi kwa bidii kwa 'quality' bila kuwa mbabaishaji

- MC , master of ceremony au msema chochote

- Wapambaji, hii ni tasnia kubwa ya peza nzuri tu inayofanywa na kina Hugo Domingo. Kubobea ni vizuri ukasomea au ukajifunza kupitia mtu anaefanya hizo kazi, muhimunkuangalia unapenda kipi.

- DJ, music supplier - hapa kuna madj, wanaokodisha miziki nakadhalika.

- Warembaji ( make up studio, beauty salon) - fursa hii hasa kwa wanawake, kuna wapambaji madada wa mjini wanatoza pesa ndefu tu wanafahamika.

- Nguo/Boutique - hii ipo crowded sana inabidi utafute 'niche' yako uweze kuwa tofauti au uwe na vitu vizuri sana na mtaji mkubwa sio rahisi kwa wanaoanza.

- Wapiga picha na video - ni tasnia kubwa tu

4. Kuongeza thamani bidhaa na kuziuza

Hapa kuna fursa nyingi za kujiajiri kuanzia kupaki mafuta ya nazi kwenye vifungashio, kubrand na kuuza. Mfano kuweka bidhaa za vyakula na matunda katika vifungashio kama unga wa lishe, ubuyu, karanga, korosho, pilipili, asali, mchele, viazi/mhogo (crisps), n.k.

5. Kuzalisha bidhaa za viwanda vidogo vidogo vya nyumbani

Mfano sanitizer, sabuni za maji, sabuni asilia zisizo na kemikali, mishumaa, toys(midoli ya kufuma), bahasha za karatasi, viatu vya kimasai, mkanda ya ngozi, mikoba ya ngozi, mabegi, n.k
Pia kuna mikufu, hereni, mazulia, batiki, vyungu, vyombo n.k.

6. Huduma/biashara mbali mbali
Duka, genge, mpesa, kampuni ya usafi, dalali, event planner, landscape,

7. Utalii
Hapa ni kuanzisha kampuni inayoratibu 'tour' mbali mbali ndani na nje ya nchi. Inahitaji mzoefu kidogo lakini haina gharama kubwa ni kupanga logistic tu. Mfano kipindi cha easter unaandaa safari ya zanzibar siku 3 au mikumi au ngorongoro unakusanya pesa unapata faida kidogo kutoka kwa washiriki na pia hoteli wanakupa 'kamisheni'.

8. Youtube - kidogo tz ipo nyuma kwenye hili pengine kutokana na sheria za nchi za kutaka watu kujisajili, lakini ni fursa pia ila mpaka kupata hela kuna msoto. Uzuri unaweza kuifanya ukiwa unafanya mambo mengine. Hapa pia kuna hizi online TV/media.

9. Ulanguzi kwenye mitandao ya kijamii - hapa ninkuwa mbobezi wa kutumia mitandao ya kijamii tu. Ukishakuwa na 'followers' basi unauza chochote unachoweza au unachoamua kujikita nacho. Faida yake huitaji kuwa na physical shop na gharama za pango. Mfano wengi wanauza simu, nguo, manukato, viatu na bidhaa za kila aina. Kanuni ni ile ile kuwa mwaminifu na vitu viwe na ubora. Unaenda dukani unapiga picha unapost, mtu akitaka unaenda mchukulia unampelekea, bila kuwa hata na mtaji unafanya.

Hayo machache nimeyafikiria kwa haraka haraka....
 
Duka, genge, mpesa, kampuni ya usafi, dalali, event planner

Asante kwa hii useful posti mkuu, i wish wote wangejibu kama wewe,lol
 
Back
Top Bottom