Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
Ni miaka minne sasa tangu tupewe kibwagizo kipya cha kisiasa cha Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya.
Je tumepata mafanikio gani kwa kauli mbiu hiyo?Je hali yetu ya Kisiasa, Uchumi, Kijamii na Kiutendaji zimepata maendeleo tangu tulipoachana na Sera za Uwazi za Mkapa?
Sikuwahi kusikia maana halisi ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya. Sikumbuki kupewa mnyumbulisho wa kusema Ari, Kasi na Nguvu Mpya zilikuwa ziwekwe wapi na kufanya nini.
Lakini mategemeo yangu kutokana na kauli hiyo ni kuwa Ari, Kasi n aNguvu ilikuwa ni msukumo mpya wa kuleta maendeleo Tanzania ambao umejaa Ufanisi, Umakini na Uajibikaji.
Kwa nchi maskini kama Tanzania, mategemeo yangu ilikuwa ni kuwa Serikali hii ya awamu ya nne, ilikuwa ije na mbinu mpya za kumwezesha Mtanzania aongeze juhudi na maarifa katika uzalishaji mali, kupunguza matumizi na kero ambazo zinadumaza na kuweka kizingiti kwenye kusukuma kwetu gurudumu la maendeleo na kuwa na mfumo bora wa uongozi ambao unang'ara kwa Uwajibikaji, Ufanisi na Umakini.
Najiuliza kwa kutumia vitendea kazi vichache tuu, je kwa miaka hii minne ya Ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya, je Tanzania tumepiga hatua gani katika yafuatayo;
Ndiyo naana nauliza je ni mafanikio gani hasa yanayopimika kwa vitendo na matokeo tunaweza kusema yamepatikana kutokana na kauli mbiu ya ari Mpya, Kasi Mpya na Nguvu Mpya kutoka kwa Uongozi wa Awamu ya Nne chini ya Mheshimiwa Rais Kikwete?

- Je Uchumi wa Tanzania, pato letu kama Taifa na Mtanzania vimeongezeka na kukua kwa kiasi gani? na katika nyanja gani?
- Je Mtanzania amepiga hatua ngapi mbele kuachana na Umasikini na kuwa na uwezo wa kujitegemea? Ama amepiga hatua gani mbele kufuta Ujinga na Maradhi?
- Je Bajeti ya Maendeleo imekua na kuongezeka kwa kiwango gani?
- Je Bajeti ya Matumizi imepungua kwa kiasi gani?
- Je deni letu la ndani na la nje limepunguzwa kwa kiasi gani? kama limeongezeka ni sababu gani zilizosababisha likaongezeka? na ni mbinu gani zinatumika kuhakikisha deni linapungua?
- Je uwiano wa mauzo nje ya nchi na uagizaji bidhaa umepungua na kurekebishwa kwa kiasi gani?
- Je ni kwa kiasi gani tumepunguza Utegemezi wa misaada na mikopo ili kujiendesha?
- Je ni mbinu gani zinapangwa kujijenga na kuwa Taifa linalojitosheleza na kuwa na Bajeti ambayo asilimia 80 au zaidi ni kutokana na uchumi wetu na pato la ndani na si mikopo au misaada?
- Je Kilimo, Ufugaji na Uvuvi vimekua kwa kiasi gani?
- Je Taifa letu limeongeza akiba ya chakula kukabiliana na njaa na ukame kwa kiasi gani?
- Je hifadhi ya mazao na usindikaji wa vyakula kwa ajili ya kuuzwa ndani na nje ya nchi kumeongezeka kwa kiasi gani?
- Je mazao yetu ya biashara, yameongezeka uzalishaji na ubora kwa kiasi gani na mauzo yake yameongezeka kwa kiasi gani?
- Je umwagiliaji na ukulima wa kisasa umeongezeka kwa kiasi gani?
- Je viwanda vyetu vimeongeza uzalishaji kwa kiasi gani?
- Je tumeweza kwa kiasi gani kuondokana na kuwa wazalishaji wa mali ghafi na kuzigeuza kuwa bidhaa kamili kupitia viwanda vyetu?
- Je ajira ngapi zimepatikana kutokana na mfumo mpya wa uzalishaji mali?
- Je Sekta za elimu na afya zimekuwa kwa kiasi gani na mafanikio yake ni yapi?
- Je vifo kutokana na maradhi kama Malaria, Kipindupindu, Ukimwi, kifua kikuu na watoto wadogo vimepungua kwa kiasi gani?
- Je lishe na chakula bora zimeongezeka kwa kiasi gani na afya za watoto na wazee zimeongezeka kwa ubora wa kiasi gani?
- Je ni wahitimu wangapi kutoka katika vyuo vyetu vyote wamepata ajira na wanafanya kazi walizosomea?
- Je tumeongeza Madaktari, Wauguzi na Watu wa Maabara wangapi?
- Je Ufanisi, Umakini, Uwajibikaji na Uadilifu umeongezeka kiasi gani serikalini?
- Je ni kwa asilimia gani mipango ya maendeleo ya Taifa ya MKUKUTA, MKURUBITA na mingineyo imepiga hatua mbele na kuleta mafanikio?
- Je Serikali imepiga hatua gani ya kuongeza ufanisi kwa kutumia Teknolojia?
- Je Serikali imefanya juhudi gani kupunguza matumizi holela ya fedha na kudhibiti uvunjaji wa kanuni za mahesabu na utendaji kama ilivyobainishwa na Ripoti ya Mkaguzi Mkuu?
- Je uhalifu umepungua kwa kiasi gani? na ni uhalifu wa namna gani?
- Je ni juhudi gani zimefanyika kujenga mfumo wa Utawala Bora wenye demokrasia ya kweli ambayo ni shirikishi?
- Je masuala ya kisiasa kama Muungano, Katiba mpya na tume huru za Uchaguzi, zimefanyiwa kazi kwa kiasi gani na matokeo yake ni yapi?
- Je ni barabara, madaraja, mifereji na vivuko vingapi ngapi vimejengwa na kuongezwa urefu ili kuboresha shughuli za Uchukuzi na Mawasiliano
- Je huduma za Reli, Bandari na Ndege kama shughuli za Uchukuzi, zimeongezeka kwa kiasi gani na zimechangia vipi kupanuka na kukua kwa maendeleo ya Taifa letu?