Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Habarini. Kuna hii ishu ya majanga ya kiikolojia ambayo mara nyingi husababishwa na binadamu na shughuli zao. mfano hapa Tanzania kuna janga la Magugu maji katika ziwa Victoria. Inasemekana yaliletwa sijui na watu gani. Pia nasikia kuna Samaki, kati ya Sato au Sangara, waliwekwa humo ziwani na kusababisha kutoweka kwa baadhi ya samaki asili.
Pia kwenye mji wa Dar kuna kunguru wanaoitwa kunguru wa Zanzibar, asili yao ikiwa Bara Hindi, hawa waliletwa Zanzibar ku;la mizoga lakini wamegeuka kuwa janga la kiikolojia. Naomba kujuzwa zaidi juu ya majanga ya kiikolojia yaliyowahi au yanayoipata Tanzania?