Gang Chomba
JF-Expert Member
- Feb 29, 2008
- 20,649
- 4,786
Key words niUnapoandika unauza mafuta ya Taa inamaana Taa ndio imetoa ama kuzalisha mafuta yale.
Neno sahihi hapo ni ''TUNAUZA MAFUTA TAA''.
.
Mkuu ukitaka kulianzisha shurti ulichanganue kwa makini na hata hyo alternative yako umekosea hilo neno limetokana na matumizi mengi yalikuwa kwa ajili ya TAA,swali vp nikinunua kerosene nikaweka kwenye jiko la mchina? Je niite mafuta mchina? Je nikinunua kerosene nikaenda kuweka kwenye jenereta? Je niite mafuta jenereta? Jipange hakuna MAFUTA TAA wala MAFUTA ya Taa,mbona petrol au diseal hawajaita mafuta gari? Coz yana matumizi mengine zaidi ya gari,kwhyo hayo mafuta yanaitwa kerosene kwa kiswahili sijui labda mtafute makii hassan(BAKITA)
Umenichekesha kweli. Ukisema mayai ya kuchemsha je? Au sweta la baridi?
Mkuu ni wazi kuwa ulifeli darasa la 7 kihalali kabisa.
Nimezungumzia mafuta Taa na wala sijataja mafuta ya alizeti wala mafuta ya karanga.
Ninachojaribu kuelezea ni kitendo cha wazalendo wengi kutumia neno ''MAFUTA YA TAA''...kana kwamba Taa ndio imetoa yale mafuta.
Najaribu kueleza kuwa kwa kiswahili fasaha ni ''MAFUTA TAA''.
ok tuambie ww ulitakaje mana umelalamika tu hujatoa matumizi sahihi ili tusiendelee kukosea
Aaah hayo ni mafuta ya kibatari au kandili,hiyo taa ni yenu nyie wenyewe,neno taa lina wigo mpana sana sina haja ya kulielezea nadhani wote mnajua.
sehemu mbali mbali hapa Tanzania nimekuta tangazo ''TUNAUZA MAFUTA YA TAA''.
Unapoandika unauza mafuta ya Taa inamaana Taa ndio imetoa ama kuzalisha mafuta yale.
Ni kama vile unapokuta mahali pameandikwa ''TUNAUZA MAZIWA YA NG'OMBE'', hapo wanamaanisha kuwa maziwa hayo yametoka kwa Ng'ombe.
Neno sahihi hapo ni ''TUNAUZA MAFUTA TAA''.
ni kweli kabisa ni mafuta taa. zamani tulikuwa tunayaita mafuta taa na sijui hili neno mafuta ya taa lilitoka wapi. au treni inavyoitwa gari moshi na si gari la moshi.
Yaani kama hivi:
Mafuta ya taa [Mafuta taa?]
Mafuta ya kupikia [Mafuta kupikia?]
Mafuta ya kula [Mafuta kula?]
Mafuta ya kujipaka [Mafuta kujipaka?]
Mafuta ya ndege [Mafuta ndege?]
Bado sijashawishika!. Lugha, hasa majina, sio lazima iwe na mantiki! Lugha ni mazoea (ya muda mrefu?) tu baina ya wanajamii katika kuwasiliana.
Hata jina la mafuta ambayo tumezoea kwa kiingereza kuyaita 'diesel' (dizeli kwa kiswahili), kimsingi linatoka na matumizi kama ilivyo 'mafuta ya taa'. Kilichoanza ni Diesel Engine (Diesel likiwa jina la mvumbuzi wa aina hiyo ya injini ya gari)....hivyo mafuta ambayo yanatumika kwenye aina ya injini ya gari iliyovumbuliwa na Diesel, wakaanza kuyaita diesel! ('dizeli' ukipenda 'mafuta ya dizeli'). Hata hivyo aina zote hizo za mafuta bado zina majina yake ya kitaalamu.