Kuna jamaa hapo anadai utafute 2M usimsikilize.
Awepo mtu wa kumsaidia kufua, kusafisha nyumba na kupika.
Hua anahitajika kuogeshwa na kukandwa (kama mama yake yupo pengine washaliongea hili).
Atatakiwa kuhudhuria kliniki, jitahidi uwepo.
Mafuta ya nyonyo unanunua ya elfu mbili tu mi sikujua nikanunua kichupa kizima hadi leo yapo na mtoto anaongea sasa hivi.
Bima kwa mtoto ni 50,400/=
Kushonana kama hana complications ni baada ya siku 40. Ila jikaze angalau miezi 6.
Hakikisha mama mtu anakula inavyotakiwa na ananyonyesha. Wengine hua hawanyonyeshi ili ziwa lisilale. Encourage kunyonyesha.
Hospitali wanasema chakula cha kichanga kitakua maziwa ya mama for six months kabla haujampa chochote. Fuatilia kama ukoo wenu watoto wana uwezo huo wa kuvumilia maziwa pekee kwa miezi 6 (kama wazazi wako upo nao karibu kimawasiliano itakusaidia) mimi mtoto alichachamaa kulia akiwa na mwezi nikaambiwa anza tu kumpa uji ndiyo mlivyo.
Pia jiandae kumsaidia kubembeleza mtoto (kama mnaishi wote) waweza rudi saa tano usiku unakuta mama mtoto kabembeleza hadi anasinzia na mtoto mikononi.
Kama unaweza kuongea naye ongea naye. Niliongea na mwanangu akiwa na siku moja, nilimuambia nilichomuambia kisha nikamuuliza "Sa nitajuaje kama umenisikia na umenielewa?" Alikua ameangalia pembeni na si unajua mtoto wa siku moja anashinda kafumba macho? Dogo aligeuka kuniangalia kisha akafumbua macho. TBF nilishtuka.
La mwisho Kama uliwahi kutaka mimba itolewe akizaliwa muombe msamaha.