Ni mambo gani uliwahi kuona kanisani kwako ya kakuacha mdomo wazi? Mimi kuzikwa mifupa ya mwanzilishi wa kanisa hilo mimbarini

Nikifa MkeWangu Asiolewe

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2024
Posts
6,944
Reaction score
14,351
Hii siyo hadithi wala story ni mwaka huu tu imetokea kwenye kanisa langu la siku zote.

Basi kulikuwa na usimikaji/kuzindua kanisa jipya tulilo changa ma hela kwa miaka kadhaa hadi mwaka huu likawa limekamilika na hatimae Askofu alikuja kulizindua kanisa hilo pamoja na kupewa hadhi ya kuwa parokia

Jambo lililo tuacha midomo wazi waumini wengi ni mambo kadhaa wa kadhaa (sita yataja yote) tukio la kulisimika kanisa lilianza saa3 asubuhi hadi saa10 jioni.

Moja ya matukio tuliyoona kwa macho ni mifupa ya marehemu aliye fariki siku nyingi kuletwa na kuzikwa kweye arutale(mimbari) Huyu marehemu ambaye kwa sasa tunamuita MT fulani kwa imani yetu.

Kulikuwa na chungu kama vile vya waganga wa kienyeji na vilikuwa na vitu kadhaa mle ndani pamoja na mkaa wa moto huku moshi mzito ukifuka.

Baada ya yote hayo kuisha kiongozi wetu wa dini yaani (.....) alipapaka mafuta na kuanza kupasugua na kupasafisha yeye mwenyewe. Na mengine mengi.

Hakika kwa haya yameniacha mdomo wazi na sio mimi tu nimejaribu kuuliza viongozi kadhaa wa dhehebu langu sijapewa jibu la kueleweka maana mimi niliona kama ni kinyume na ukristo.

Wakuu nahitaji kuuliza maana nilijua najua vitu vingi kwenye imani yangu kumbe bado kabisaaa ni mtoto.je hii ina ulazima gani na kwanini ifanyike hadharani na mc akitangaza hadharani kwenye vipaza sauti na watu wasio sali dhehebu letu wasikie na kujua kinacho endelea?

Je, wewe umewahi kuona kitu ambacho kilikuacha mdomo wazi na maswali mengi .
 
Ndugu yangu alimkuta mchungaji na mke wake wanaroga kanisani (alikua anaenda ibada ya usiku - walokole) walivomuona wakamwambia usije kanisani hadi zipite siku 7 na usimwambie mtu yeyote haya uliyoyaona hapa, akahisi wanatania.

Kesho kutwa yake alienda kanisani (ilikua ijumaa wanakati wanaroga, jumapili akaenda ibada ya jumapili), alivotoka kanisani akawa mwehu ghafla, akawa anakimbia kimbia tu hadi akaanza kusahau watoto, akafungwa kamba na kuanza kuombewa (mme wake alikua hajui chanzo ni nini). Wamehaingaika nae kwa muda mrefu, ikabidi apelekwe kwa waganga wa kienyeji, alikuja kupata unafuu baada ya miaka miwili mbele ndiyo kusimulia yote.
 
Halafu utasikia wanasema waislamu ni washirikina.

Kwa asili muafrika yake ni tunguri tu, hizi imani nyingine ni maigizo.
 
Mkuu hayo ni mambo ya kabisa katoliki, ukiona kabisa Linaitwa parokia ya mtakatifu "yuda thadei" ujue Kuna mifupa ya huyo mtakatifu altareni, huo ni upagani kama upagani mwingine eg kuombea wafu,kuabudu sanamu nk..
Kuna vingi vinafanyika kinyume na biblia,
 
Ungeelezea hadi mlivyoenda uwanja wa Ndege kwa maandamano kupokea hiyo mifupa. hahahaha....

RC Area A!
 
Ata askofu akifa Kuna kaburi lake kabisa ndani ya kanisa apo jimboni.tuache na imani yetu
 
Duuhh haya mambo siwezi kataa
 
Hii Nimeona kwa macho yangu mchana kweupe.
 
Mboni umetupiga kamba?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…