Ni mazingira yapi na wakati upi DPP anaweza kuwasilisha Nolle Prosequi Mahakamani

Ni mazingira yapi na wakati upi DPP anaweza kuwasilisha Nolle Prosequi Mahakamani

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
Wakuu Habari Ya Mawio.

Wakuu Neno Nolle Prosequi ni neno la kilatini linalomaanisha hati ya kisheria ya nia ya kutoendelea na mashtaka dhidi ya mtuhumiwa Yaani To be unwilling to pursue

Sasa Hati hii huwasilishwa mahakamani na mwendesha mashtaka Kwa Maana ya Dpp au mlalamikaji.

Kwa hapa nchini Mwendesha Mashataka (DPP), anayo mamlaka kisheria chini ya kifungu cha 91 (1) cha sheria ya makosa ya jinai (CPA) kuwasilisha hati hii pale anapoona inafaa kufanya hivyo.

Sheria haimpi wajibu wa kueleza sababu za kuwasilisha hati Hyo

Kisheria makosa ya jinai yanapaswa kuwa na ushahidi wa kutosha na usio na shaka hata chembe ili kumtia hatiani mtuhumiwa.

Hivyo DPP anapoona mapungufu kwa kiwango chochote anaweza kuwasilisha Nolle.

Hivyo haimaanishi kila mtuhumiwa anayeachiwa kwa hati hii hajatenda kosa bali kukosekana kwa ushahidi usio na shaka.

Wakati mwingine Nolle Prosequi huwasilishwa Mahakamani na mtuhumiwa kuachiwa huru ili kuipa ofisi ya Dpp nafasi ya kufungua kesi mpya dhidi ya mtuhumiwa pale ushahidi unapokamilika badala ya mtuhumiwa kuendelea kukaa mahabusu.

I stand to be Corrected[emoji120][emoji120]

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
I am sorry, kwa Tanzania yetu DPP anaweza fanya akili yake inavyomtuma maana hakuna utawala wa sheria na hakuna wa kumwajibisha in case!
 
Tanzania ni nchi ya hovyo sana.

Watu wanabambikiziwa kesi sababu tu sio mwana CCM.
 
I am sorry, kwa Tanzania yetu DPP anaweza fanya akili yake inavyomtuma maana hakuna utawala wa sheria na hakuna wa kumwajibisha in case!
Mkuu Ujue Circumstantial evidence ( kuwapeleka alikozikwa na kuwaambia watu mama kasafiri hayupo) could be corroborated by expert opinion na police statement.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom