Ni mechanism gani hutumika kuwasha pikipiki kwa kusukuma?

Ni mechanism gani hutumika kuwasha pikipiki kwa kusukuma?

Offshore Seamen

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2018
Posts
5,489
Reaction score
14,091
Pikipiki katika kuwasha unaweza ukatumia njia ya Kick Starter, Electric Starter na kusukuma.

Swali langu lipo katika njia ya kusukuma ambapo mtu anayewasha anaweza akakaa katika pikipiki wakati huo akiwa ameweka gear namba 2 na kabana klachi baada ya kusukumwa kidogo huinuka na kukaa kwa ghafla na kuachia klachi kitendo hiki huwa ni wakati mmoja. Na hapo pikipiki inaweza ikawaka endapo vitendo vitafanyika kwa usahihi na timing ya kuachia klachi.

Au dereva wa pikipiki akiwa peke yake anapowasha kwa kusukuma huweka gear namba 2 kisha hubana klachi na kuisukuma baada ya hatua chache akiwa upande wa pembeni anarukia kiti ghafla na kukandamiza chini kisha kuachia klachi na pikipiki huwaka.

Je, ni mechanism gani au kuna uhusiano gani wa kuwasha pikipiki na mshtuko wa ghafla kukaa katika kiti ili pikipiki iwake?
 
Offshore Seamen,
Zote njia ulizotaja ziko sawa, hakuna utofauti, lengo ni kuizungunsha injini kwa nguvu ya kutosha iweze kuwaka tu, eidha umetumia mguu , umeme au gurudumu kwa kuisukuma.
 
Zote njia ulizotaja ziko sawa, hakuna utofauti, lengo ni kuizungunsha injini kwa nguvu ya kutosha iweze kuwaka tu, eidha umetumia mguu , umeme au gurudumu kwa kuisukuma.
Kwenye njia ya kuisukuma ni kwanini baada ya kuisukuma tunaiongezea kwa kuikalia ghafla kwenye kiti.
 
Kwenye njia ya kuisukuma ni kwanini baada ya kuisukuma tunaiongezea kwa kuikalia ghafla kwenye kiti.

Sasa unataka aiwashe akiwa hajakalia ili ikiwaka imuache anagalagala? Kumbuka kwamba kwa njia hii ya "jump start" ikiwaka kwakua iko katika gia namba 2 lazima itatembea kidogo mpk pale inapochanganya dereva anarudisha "control" kwa kutoa gia na kusimama. Sasa hayo mambo ni ngumu kidogo kuyafanya iwapo hajapanda(kuvuta klachi, kupangua gia na kutia breki)

Na hio sio kwenye pikipiki tu,hata kwenye magari ya kusukuma endapo hauna mtu wa kusukuma na ukasukuma mwenyewe dereva mziki huwa unakuja kwenye kuidandia hio gari na kuiwasha(mara nyingi inakua free, unadandia,unakanyaga klachi unaweka namba 2 hapafu "unaibutua"......)
 
Sawa mkuu
 
Kwenye njia ya kuisukuma ni kwanini baada ya kuisukuma tunaiongezea kwa kuikalia ghafla kwenye kiti.
Ishu ni hivi ili tairi liweze kuizungusha injini grip kati ya tairi na ardhi inatakiwa iwe ya kutosha hvi kwakua pikipili ni nyepesi kwa nyuma, mtu urukia ili kuongeza uzito na kuifanya tairi iwe na mgandamizo wa kutosha kwenye ardhi ili tairi iweze kuizungusha injini.
 
Sasa unataka aiwashe akiwa hajakalia ili ikiwaka imuache anagalagala? Kumbuka kwamba kwa njia hii ya "jump start" ikiwaka kwakua iko katika gia namba 2 lazima itatembea kidogo mpk pale inapochanganya dereva anarudisha "control" kwa kutoa gia na kusimama. Sasa hayo mambo ni ngumu kidogo kuyafanya iwapo hajapanda(kuvuta klachi, kupangua gia na kutia breki)

Na hio sio kwenye pikipiki tu,hata kwenye magari ya kusukuma endapo hauna mtu wa kusukuma na ukasukuma mwenyewe dereva mziki huwa unakuja kwenye kuidandia hio gari na kuiwasha(mara nyingi inakua free, unadandia,unakanyaga klachi unaweka namba 2 hapafu "unaibutua"......)
Nitakupinga kidogo kwenye swala la kuidandia.
Dereva lazima aidandia ili iwe nzito kuruhusu mfumo wa injini uzunguke badala ya tairi kuburuta chini/break ya ghafla huku zoezi lake likifeli
Kumbuka unapowasha pikipiki kwa kutumia eidha starter au kick, ni lazima ubane clach ili kutenganisha mfumo wa gearbox na injini kisha baada ya kuwaka ndipo unaweka gear ili uachie clach uondoke.
Sasa bas unapokuwa unaforce kuwasha kwa kusukuma, unahitajika uweke gear kwanza alafu ubane clach ndipo usukume kisha uachie clach huku ukiendeleza mzunguko wa injini iliyo na gear tayari kwa lengo la kuilandanisha injini na mfumo wake wa gear.

Sasa kile kitendo cha kuirukia pikipiki muda uleule unapoachia clach ni tendo lenye ushirikiano kuanzia kwenye tairi, injini na gearbox kwa pamoja/yaani kama hutoirukia pikipiki muda wa kuachia clach, moja kwa moja tairi ya nyuma ya chombo chako itajiburuta kama vile umebana break kwa sababu uzito wa hiyo pikipiki hautotoshea kuweza kushika chini/tairi lililounganishwa na mfumo wa injini kuweza kuzuia mserereko ili injini iweze kuwaka kikamilifu.
Bila tendo la kuirukia pikipiki ili iwe nzito kuweza kuwasha injini, tutaona matokeo ya tairi ya nyuma kushika break kisha pikipiki kusimama. Pia kumbuka sio pikipiki zote hurukiwa ndipo ziwake [emoji23]nyingine hata kwa kuishtua sehemu tambarare tu inawaka,,,, hii inategemea na speed uliyoisukuma pikipiki au injini na injini.

Hivyo tunaweza kusema ingekuwa sivyo, basi tungeweza kusimamisha pikipiki kwa kutumia stendi kubwa kisha tuweke gia, tubane clach, tuzungushe tairi la nyuma kwa mkono alafu tuachie clach ghafla pikipiki iwake.

Point ya muhimu tunapofosi kuwasha injini pasipo kutumia mota ya pembeni, ni lazima injini husika ihitaji nguvu inayoizidi ili injini hiyo ishindwe kubishana na nguvu hiyo iwake..

Pia hata tunapowasha injini kwa kutumia mota ndogondogo za pembeni, inahitajika mfumo wa injini hiyo utenganishwe kwanza na gearbox. Nje ya hapo tutatukuwa tunaforce jambo ambalo injini hiyo itahitaji nguvu kubwa kuizidi ndipo iwe kwenye rotation yake ya kawaida.
 
Back
Top Bottom