Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

Camilo Cienfuegos

JF-Expert Member
Joined
Apr 23, 2015
Posts
18,960
Reaction score
67,654
Yaweza kuwa ni kwa matokeo ya kushangaza au ya kawaida tuu, Yaweza kuwa ni burudani ya pasi na udambwi dambwi wowote ule.

Mechi zangu mimi ni hizi.
1.Germany 7-1 Brazil kwenye World Cup.

2.Man Utd 2-0 Arsenal. Hii mechi inajulikana kama Battle of the Buffet, ulikuwa mwisho wa Unbeaten record ya Arsenal. Mechi ilijaa undava wa kila aina.

3.England vs Greece. Kufuzu World Cup 2002, ambapo Waingereza walipata bao la jioni kabsa toka kwa freekick ya Beckham na hivyo kufuzu.

4.Barcelona 3-1 Man Utd. Hii ilikuwa fainal ya Champions League ambapo Barca walikuwa ktk ubora wao hali iliyomfanya Ferguson kutetemrka kwa nyakati fulani.

5.Taifa Stars 0 -1 Msumbiji. Kufuzu mataifa huru mwaka 2008.Nani amemsahau Tiko Tiko?

Kwa upande wako ni mechi zipi hutozisahau??
 
Mechi kati ya Chelsea na manchester united mwaka1999, wakati huo man ilikuwa man kweli! Lakini man siku hiyo iliangukia pua, ilipigwa goli 5-0! Hiyo ndiyo chelsea, wale wanaodhani chelsea ilianzia kutamba baada Abramovich kuinunua watakuwa ni watoto wa juzi sana!
 
Chelsea 3-2 barca! Nusu fainali ya pili UEFA mwaka ule chelsea walibeba ndoo ya UEFA!
 
Arsenal 2-1 barcelona
villa mapema kipindi cha kwanza anampiga tobo kipa wa arsenal
kipindi cha pili Robin van Pussy anasawazisha kwa bonge la kombola kipa analikwepa pale sijui wenger anafikiria nini pasi ya kwanza ya pili ya tatu mguuni kwa van persie kama anapiga vile kumbe Arshavin ameingia anamuomba anapiga bonge la kamba nyavu ndogo anajifunika na jersey yake usoni kumbe mpira unaanza kati

hiyo emirates barca isiyofungika hiyo
 
The special one beat the special team(Intermilan vs Barca),semi final Uefa champions league,2010. Barca anakufa tatu.Cambiasso,Motta,Sneijder miguu imejaa kama ndoo za litre 10,sijawahi kuona viungo waliokua wanazingatia,wanakaba kama hawa na kwa ujumla wao siku hiyo kilometres walizokimbia uwanjani ni kama kutoka Dar mpaka nyumbani Shinyanga.Bonge moja la gemu
 
Man U 2 Bayern Munich 1....Final ya UEFA Champions League (Enzi hizo ilijulikana hivyo, sasa ni Champions League)

Hapo ilikuwa 1999 tulipochukua treble.
 
Duh hii mechi siwezi kusahau kabisa nakumbuka jinsi ilivyokuwa na ushindani mkubwa Bayern ilikuwa imejihakikishia kuchukua ndoo.Super sub na Teddy walifanya mambo dakika za nyongeza Samwel Kuffor alilia kama mtoto mdogo.Man ya wakati huo ilikuwa kiboko mpira ilikuwa ni dk 90 nje ya hapo matokeo yaliweza kubadilishwa wakati wowote.

Man U 2 Bayern Munich 1....Final ya UEFA Champions League (Enzi hizo ilijulikana hivyo, sasa ni Champions League)

Hapo ilikuwa 1999 tulipochukua treble.
 
daaah kweli barcelona noma yan wengibwao wanafurahi kwa kuifunga Barca ila saf sana kwani mnadhihirisha kuifunga Barca si kitu rahisi yan.kuifunga ni ndoto
 
Man U 2 Bayern Munich 1....Final ya UEFA Champions League (Enzi hizo ilijulikana hivyo, sasa ni Champions League)

Hapo ilikuwa 1999 tulipochukua treble.

Msimu huu ndio ulionisababisha niipende man u na wakati huo huo kuichukia...na mpaka Leo bado naichukia sana
 
Hii ilikuwa kiboko maana hadi half time Liverpool alikuwa kafungwa 3~0.alivyoingia aliwagonga na kombe akapewa

Nilikiwa team AC Milan, niliaje siku hiyo. Sitokaa nisahau maisha yangu yote
 
world cup 2010 south Africa asamoh Gian anakosa penalt yaani hii mechi niliumia kumbuka ilikuwa tuweke history timu ya Africa kutinga semi final
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…