Ni mechi zipi za soka hutozisahau kamwe?

Machester Derby 2011? "Why Always Me".

United 1 vs 6 City. Nina washkaji kadhaa wa United na wanaongea hatari, i trolled them katika kiwango ambacho sijawahi kufikia hata nusu.

R.I.P my homeboy Lexa Julius, hardcore United fan i knew.
 
Nimeangalia tena rekodi zangu, Italy alifungwa kwa matuta, aliyekosa penati ni Roberto Donadoni ambaye baadae alikuja kuwa kocha wa Italy kwenye Euro 2008

Upo sawa mkuu. Kuna kitu waliita no 17 ya mkosi. Donadoni alikuwa akivaa jezi no ngapi? Angalia record zako vizuri...hii kitu iliandikwa mpaka na gazeti la chama wakati huo UHURU.
 
world cup ya 2014 match ya Belgium na USA, nadhani ndo ilikuwa one of my fav matches kwa world cup ile
 
Kuna game ilikuwa world cup 2006 km sikosei kati ya ureno na uholanzi..daa ile game sitokaa nije kuisahau..ilinikosha si kidogo
 
'09 Fifa Confederations Cup final.

United States vs Brazil. Hiyo comeback ya Brazil, whoo!!

Hiyo mechi umenikumbusha bro. Kaka alipiga mpira nadhani ilikuwa Maximum pale, alifunga goli likakataliwa aisee. Hapo ndio ninapo ona umuhimu wa GLT (Goal Line Technology)
 
Kama akucheza na bayern hlo kombe 1 la uefa analo limiliki alilichukua kwa nani fainal..??
mkuu hukuandika bayern uliandika bayer ambayo ni bayer leverkusen, jitahidi kutofautisha hizi timu mbili mkuu
 
UEFA Champions League final 2008 pale J. Terry anapoweka kitambaa chake cha ukapten halafu anateleza kwa tuta aisee
 
Mimi hata sitaki ziongelea maana machungu sana
 
msiwe mnabishabisha tu kama hamjui kitu nyambafu

wewe ndo hujui kuna vi2 unaweza ona ni typng error ya nn unaleta ubishi wa shule ya msingi...au ni shabiki wa man u nini...!!???
 
nakumbuka Euro kama ya 2004 kama sja kosea....france vs england ad.dakika ya 90 england wanaongoza 1-0 henrry akawakimbiza kawekwa chini faulu zizuu akaingia kambani...dakika 1 mpira kuisha henrry kawakimbiza tena robson kamweka chini..zizzou penalt..kamba...ikawa 2-1.
 
Man City vs QPR ambayo Aguero anafunga goli la 3 na kuwa 3-2 mwaka 2012 na kuchukua Ubingwa hii mechi sitomsahau Joe Barton kwa rafu kwa Tevez wakapungua wakatawala gemu. Pia Jibril Cisse walikuwa wanawania counter attack tu.
 
Liverpool vs Westham Capital One cup final. Comeback ya Liver ilikuwa noma. Gerard hatasahaulika pale
 
Nusu fainali ya uefa man u ya kina Beckham, nestrooy vs real Madrid ya enzi ile ya Ronaldo de lima, Figo, Zinedine, makelele, Roberto Carlos kocha del Bosque , man 4 real 3,Ronaldo alimpiga kanzu barthez na kumfunga. Ferguson aliita usiku wa soka
 
Cameroun Vs Argentina,
Argentina ilikuwa full mziki wa kina Maradona, Claudio Cannigia nk huku Cameroun ikiwa na kina Thomas Nkono, Makanaki, Roger Milla, Emmenuel Kunde, Louis Mfede, Francoi Biyiki nk

mwisho wa mechi Argentina walilala 1-0, huku wachezaji wawili wa Cameroun wakitolewa nje kwa kadi nyekundu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…