Elections 2010 Ni mgombea yupi mwenye nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu (Ubunge) jimbo la Kawe?

Elections 2010 Ni mgombea yupi mwenye nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu (Ubunge) jimbo la Kawe?

MwanaHaki

R I P
Joined
Oct 17, 2006
Posts
2,401
Reaction score
707
Waungwana,

Mpaka sasa, Jimbo la Uchaguzi la Kawe lina wagombea wafuatao wa Ubunge, ambao ndio wanaosikika.


  1. Angela Kizigha (CCM)
  2. Halima Mdee (CHADEMA)
  3. James Mbatia (NCCR-Mageuzi)
Kinyang'anyiro hiki kinaonekana kuwa zaidi kwa vyama hivi vitatu, ambapo umejitokeza ushindani mkubwa.

Tetesi zinasema kwamba wakazi wengi jimboni wanamtaka zaidi Halima Mdee, huku nyingine zikisema kwamba huenda James Mbatia akashinda.

Wako watu wengi wanaosema Angela Kizigha hana la kuongea, na akiwa kwenye kampeni anashindwa kuongea, anakwepa kujibu maswali anayotupiwa. Inadaiwa kwamba yeye hayuko mbali na Hawa Ng'umbi, ambaye CCM imetamka kwamba italazimika kutumia nguvu nyingi kurekebisha hali ya hewa aliyoichafua wakati alipopandisha jazba kwenye mdahalo wa TBC1, ambapo Hawa alipandisha jazba na kumjibu mwandishi wa habari aliyemwuliza maswali kuhusu tuhumba mbali mbali dhidi yake.

Ningependa kupata maoni yenu. Nani atashinda?

Asanteni.

-> Mwana wa Haki
 
siyo la kuuliza hili....
ubungo=Mnyika
kawe =Mdee
nimesahau kigambo = mama yangu Matilda Komu
 
Mimi naona Halima atashinda lakini Mbatia naye ana hoja zake za msingi. Ndio maana nikaulisaaaaaa!
 
Angela Kizigha hajulikani. Mwenye taarifa zake azilete tumjadili. Hana skendo kweli huyu? LOL
 
Back
Top Bottom