Mhafidhina
JF-Expert Member
- Feb 6, 2008
- 549
- 23
Pole sana.
Ndugu Dr. Saikos One, nafikiri jibu la swali lako unalo mwenyewe kupitia kichwa cha habari cha mada yako "Ni mimi tu ninamkosi na wachaga au ndiivyo walivyo?"
Hapo nilipoweka nyekundu ndo jibu lilipo. Pengine wewe ndio una mkosi...!
Waheshimiwa Wana JF,
Mimi Naomba msaada wenu wa Ushauri ili niondokane na hii hali ya utumwa wa kupenda. Kuna mtoto mmoja wa kichaga simuelewi nini lengo lake! Nilikuwa na mahusiano naye toka mid. April, sijahusiana naye kwa tendo takatifu hadi sasa. Mie nipo huku napiga box, yeye alikuwa huko Waja leo na sasa yupo DSM lakini kilichonishangaza awali alikuwa akiniambia kuwa next week or kesho naenda DSM kuna kazi nimetumwa kuifuatilia.
Baada ya hapo safari zikazidi, mawasiliano hadi mie nianze, mbaya zaidi kanistukiza ghafla eti kahamia kikazi Dar, na hapo napewa taarifa wakati tayari yupo DSm anasema "aaa haa nipo ofisini kazini, nimechoka hata kutuma msg muda sina"! Je ndio mapenzi ya wachaga yalivyo? Najiuliza au sababu mie sio mchaga? Ni kitu gani hasa wanawake wa kichaga wanapenda zaidi toka kwa wanaume ukiachilia mbali mapenzi? Mwisho naomba kuuliza hivi kwanini wanawake wengi wa kichaga huwa hawaolewi haraka na utakuta umri unakwenda yeye bado haolewi lakini mali ukiomba anagawa kama kawaida lakini ndoa hazifungwi?
plse wana JF naomba mnijuze ili kama vipi nihame huko migombani na nisipende tena hii kabila!
Mkuu sioni hayo matatizo ulionayo na huyo msichana yana husiana vipi na uchaga wake .Thread kama hii ndio zinaletaga chuki za ubaguzi.Wewe unatatizo na mchaga mmoja halafu tabia yake ndio una generalize kwa wachaga.
Halafu unajiita doctor, Shame on you!
fimbo ya mbali haidedish snake .
pole kaka bt she iz away n
full in love wth somebody else
kubali hali,meza maumivu then move on
pole bt ukweli ni uo ( ANGEKUWA ANAKUPENDA KWELI ANGEKUSHIRIKISHA KILA KITU NA ASINGEKUWA MZITO KIMAWASILIANO ITS JUST LABDA KAJA UKU DAR KWA JAMAAA YAKE SO HAWEZ KUWA ON NA MAWASILIANO JUU YAKO)
Inakuuma nini sasa, kwani wewe huko uliko unaishije? Na yeye atajua vipi kama hauna mahusiano na mtu mwingine? Ndo maana na yeye anaamua kufanya mambo yake napia kua na mtu mwingine then achague yupi yuko serious. Hajakuacha ila amekupiga bench tu kidogo acheki vikimshinda huku atakurudisha mzigoni. Istoshe nyie pia hamueleweki unaweza mkalisha mdada wa watu wee anakusubiri tu then unarudi unaoa mwingine, so fikiria haya halafu maumivu yataisha. Ukizingatia ukute hata perfume hujawahi mtumia ni story tu kwa sim kila baada ya wiki. Ukirudi katafute kijijini.
Endelea kupiga box tu - Wazuri wapo wengi!
Mkuu,
Unajua philosophy ya mapenzi ni pana sana. Haina maana kuwa mwanamke ukimnunulia perfume au Rav4 ndio unampenda au yeye anakupenda @! Pia ile dhana kuwa mwanamke wa kudumu katika ndoa ni yule wa kijijini hiyo dhana nayo imepitwa na wakati mkuu. Wale wa jana sio wa leo Kiongozi wangu!
Wanasema mapenzi ni kupendana so haijalishi we ni wa wapi au unanini hivyo ndio mimi nijuavyo au siku hizi mapenzi ni PESA??? plse wapendwa naomba niwekwe wazi juu ya hili.
Mkuu,Pole sana
Mkuu nadhani umenisoma sivyo ndivyo. Kumbuka Tanzania ina makabila zaidi ya 120 lakini wachambuzi wa mambo ya mahusiano wanajua almost kila kabila lina tabia zipi kuu katika suala la mapenzi au ndoa. Binafsi sikuwa na maana ya kuponda wachaga ila nilikuwa namaanisha msichana niliyekuwa nimempenda ni wa kabila hilo ili niweze kupata mchango wa mawazo ulio na reference sahihi ya mtu maeneo atokayo kuliko wadau waanze kuuliza huyo ni wa wawapi.
Anyway, kama kuna watu nitakuwa nimewakwaza kwa hilo sina budi kuadmit kuwa sitarudia kufanya hivyo bali kwa sasa naomba mawazo yenu ili yaweze kunipa mwanga wa nini cha kufanya.