Ni msemo mtamu sana lakini ni hatarishi

ndayilagije

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2016
Posts
7,491
Reaction score
8,304
Hi.
Kuna msemo mmoja huwa ni amazing sana kutamka mdomoni mwako. Unakufanya ujisikie god/godes. Lakini unawasha sana masikioni mwa muambiwaji. Unajenga chuki,unaharibu uhusiano,unavuruga familia,unakimbiza wateja. Ni huu "kama hutaki acha" usipende sana kuutumia.
 
Alafu msemaji anakuwa kama hajawai kupata shida kabisaaa maishani mwake. Ila kanakera sana hako kasentesi
 
Alafu msemaji anakuwa kama hajawai kupata shida kabisaaa maishani mwake. Ila kanakera sana hako kasentesi
Nahisi ni ukosefu wa mbinu za kutatua migogoro..wanakatumia kama defense mechanism tu ila kanawasha sana. Ukinijibu hivyo dukani naondoka tu.
 
Kuna Muuza nyama alinitusi hivyo hivyo enzi za nyuma kidogo.
"Kama hutaki, nenda zako" akaongeza na mengine.
Hakujua kama nyumbani wanapenda nyama sana na mimi ndiye mtoto pekee niliyekuwa naagizwa.

Nilienda kununua karibia mara kibao kwa jirani yake, ilibidi aanze kunisemesha kwa upole na heshima siku zilizofuata.

Nahisi ilikuwa tabia yake, kila siku nyama zake zilibakia kibao. Naona hata wengine walimsusia.

Mwisho alifunga duka lake.
Kauli njema kwa wateja hupendeza zaidi
 
Hahaaahaaaa......[emoji13] [emoji13] [emoji13]
Ulichangia kufilisika kwa muuza nyama
 
Lugha za kshenzi!kama anakupa bure vile,kumbe unanunua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…