Ni mtu gani (ID) hapa JF akicomment kwenye post yako au ni comments za aina gani hukupa raha?

Mtini

JF-Expert Member
Joined
Apr 28, 2011
Posts
1,492
Reaction score
2,361
JF pamekuwa mahali pa burudani sana, wengi wetu hata tukiwa na stress huwa tunakimbilia huku. Wabarikiwe wote waliaokuwa sababu ya kuanzisha jukwaa hili.

Baada ya salamu kama wafanyavyo wabunge pale mjengoni sasa niingie kwenye hoja. Hapa JF kuna watu wa tabia au watu wa aina nyingi na hata aina ya comments zao huwa ziko tofauti sana, ila yote kwa yote huwa ni burudani tosha sana. Kuna wakati mimi hufurahia tu kusoma comments za wadau humu, nyingine huwa ni za hoja, vichekesho, mafumbo na hata za kumnanga mwenyikiti wa kijiji chetu.

Binafsi huwa nafurahishwa na utaaluma (utaalamu) wa wanajukwaa katika kutumia lugha hii adhimu kumnanga mwenyekiti wa kijiji chetu. Kuna kautaaluma fulani hivi wadau wanakaweka basi hapo huwa ni burudani tosha. Namkubali sana bwana Njaa, Nyani Ngabu japo tokea akamatwe na corona kapotea, Sky Eclat, Vuta Nikuvute, na yule bibi japo simpendi kidogo maana kazidi mno kuzipamba juhudi, orodha ni ndefu bila kumsahau mzee wa kujivukiza kwa mitishamba aka Mshana Jr
 
bila kumsahau mzee wa kujivukiza kwa mitishamba aka Mshana Jr [emoji848][emoji44][emoji119][emoji30][emoji12][emoji12][emoji12]

Jr[emoji769]
 
Burudani inaongeza zaidi ukikuta umekuta comment ya mtu ulietamani achangie japo kidogo unatulia kusoma ujue ameandika nini
 
Member yeyote ambaye tuliwahi kukwaruzana/kutofautiana kwa namna moja ama nyingine wakati wa mijadala mbalimbali humu jukwaani. Huwa nikiona mtu huyu ame'like post yangu, ame reply kwenye uzi wangu huwa nafurahi na kufarijika.
 
Naona bado hajafika kwenye huu uzi, akija nitalike comment yake.
 
Mie binafsi nawakubali wote...sanasana wale ninao zinguana nao inbox halafu huku tunaongea vyema kama hakuna kilichotokea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ