Ni muda muafaka tuwe na vyuo kila mkoa

Rebeca 83

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2016
Posts
15,136
Reaction score
32,268
Hello wanajamii.

Kunususru janga la ajira kwa vijana.

Ni kuwa na vyuo kila mkoa/mji.

Vyuo hivi vijengwe kutoa elimu ambayo sio general, bali specific kutokana na rasilimali zilizopo/zinazopatikana kwa wingi kwa sehemu husika.

Kwa mfano, labda Mwanza kunapatikana samaki,vyuo vya uvuvi na biashara ndio vijengwe huko,halikadhalika labda Tanga kunapatikana matunda, elimu juu ya kusindika matunda na kuuza kama biashara itolewe Tanga, n.k

Mimi nahisi pengine tukifanya hivi vijana wataona fursa zilizopo karibu/kwenye miji yao na kubaki huko,

Its high time serikali i tackle unemployment kwa kuangalia resources zilizopo kila mahali,na ku enable vijana ku exploit resources hizo.

KIngine nachoona kila mkoa ujisimamie kimapato na miradi yake, itastimulate creativity/innovation kwenye fursa na changamoto zinazokabili mkoa kama mkoa.

Nimeongea hivi sababu kuna sehemu kama huko Kondoa,Tabora na Kusini mwa Tanzania ni kama kumesahaulika.

Na wakati kuna Asali, Korosho n.k

Pia tunashuhudia ma Fly over, madaraja sijui kwa Mfugale hapa Dareslaam, hujawahi kusikia vitu hivi Mafly over huko mkoani.

With 65% of Tanzanians live in rural areas, its time Infrastructure iwe invested huko, na sio Dar es Salaam(msinipopoe ni ukweli)

Karibuni
 
Serikali ina mpango madhubuti baada ya kumaliza ujenzi wa hospital mikoani inampango wa kujenga vyuo vya VETA kwenye kila mkoa so nadhani labda haukuwa unajua.

Actually Rais alisema phase ya muhimu ni kila mkoa then itatafutwa pesa ili kuangalia zile wilaya ambazo zina maendeleo na uhitaji basi watajenga kila wilaya.
 
Hapo ni kama unapendekeza kua na serikali za majimbo au federal government system, kama iliopo US Germany, China Nigeria SA nk

Hapo maendeleo ya tafanyika kulingana namahitaji ya eneo husika, ila hilo serikali ya CCM au Chadema ndo hawataki kulisikia wote wanajificha kwenye sabb za kuleta ukabila na Ubaguzi, jambo ambalo sio sahihi, hu mfumo wa kua na republican government moja imesha pita na wakati, manaake ma dictators ndo walipendelea huo mfumo wa centralised governance. Tz haiwezi kupata maendeleo kwa mfumo wa aina hi eti Raisi alioko Dar ndo amue kipi kifanywa kule Ngara au Miswingwi.
 
1. Kwa hiyo unapropose tuwe na serikali ya majimbo? Federal states na sio centralised gov't? Kuna mikoa itakuwa na maendeleo 200% na mingine 20%.

2. Vyuo, labda vocational training institutes. Vyuo vukuu havina tija kwa taifa. Graduates wengi wamejaza nadharia vichwani lakini practicals hakuna kitu.
 
With 65% of Tanzanians live in rural areas, its time Infrastructure iwe invested huko, na sio Dar es Salaam(msinipopoe ni ukweli)
siku zote watu huja mjini kula raha na sio vice verse
 

No 2, why do you think so?? embu expound please
 
Unahoja ya msingi, focus uwekezaji $$$/ Tsh iwe veta 80% wakihitimu na mkopo tools set basic, rest fani nyingine.
 
No 2, why do you think so?? embu expound please
Vocational training institutes ndio zina tija kwa taifa coz zinaandaa vijana kuingia mtaani na ku exploit opportunities, universities zinawaandaa vijana kutembeza bahasha. Wewe si umesema vijana wafundishwe kukamatia fursa, au nimeelewa vibaya
 
Vocational training institutes ndio zina tija kwa taifa coz zinaandaa vijana kuingia mtaani na ku exploit opportunities, universities zinawaandaa vijana kutembeza bahasha. Wewe si umesema vijana wafundishwe kukamatia fursa, au nimeelewa vibaya
Nimeuliza sentence yako ya pili,Luna sehemu zitakua na maendeleo zaidi ya nyingine
 
Nimeuliza sentence yako ya pili,Luna sehemu zitakua na maendeleo zaidi ya nyingine
Of course kuna sehemu zitakuwa na maendeleo zaidi kwa sababu ya resources zilizopo. Kuna mikoa ina limited resources, na wewe ume suggest tusiwe na centralised gov't, unataka majimbo ambayo kimsingi yanasimamia rasilimali zilizopo na kuwanufaisha watu wa eneo husika.
 
Si ndo VETA mkuu sasa hivi ukienda VETA unakutana na watu wamemaliza bachelor wanasoma huko jinsi ajira zilivyokuwa ngumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…