Kujilinda dhidi ya taifa gani kubwa mkuu?
Je umekagua vikosi vya majeshi ya ulinzi ukakuta wamezubaa kama unavyofikiria?
Ni kweli tumezidisha mapambio kupitiliza,mpaka inakera.
Lakini hatuwezi kuendelea kiuvumbuzi kama kila mvumbuzi anawekwa ndani kama criminal.
Mtu akigundua kutengeneza gobore badala ya kumpeleka jeshini akajiendeleze kitaaluma.
Sisi tunampeleka magereza akalime bure.
Mtu akigundua kutengeneza gongo la kienyeji anakamatwa na kufungwa eti pombe haramu.
Badala ya kumuendeleza ili aiboreshe kwa teknolojia ya kisasa zaidi.
Mtu anayeruka na ungo usiku tungewashauri ili wakubali kuiweka wazi teknolojia yao badala ya kuwaua kwa mapanga usiku.