Hata hivyo kwa ukatili na kiburi walichofanyiwa awamu hii, somo litakua limewaingia. Walitakiwa waweke sharti tangu mwanzo la kususia huu uchaguzi iwapo kusingefanyika marekebisho ya msingi!
Lakini hilo halikufanyika. Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa 2019, na ule wa marudio ya wale Wabunge na Madiwani njaa, kauli za kutatanisha na kukatisha tamaa za Rais aliyeko madarakani, Spika wa Bunge, nk.
Vyote hivi vilikua ni viashiria tosha ya kwamba kutakua na maigizo yanayoitwa uchaguzi, lakini hawakutaka kuelewa na kuchukua hatua. Watakua nje ya Bunge sasa. Ni wakati wao sahihi kupigania mabadiliko ya kweli.
Tumerudishwa miaka ya 1960's - 1970's! Hakika ni jambo la kusikitisha sana.