Ni muda sasa vijana kwa wakubwa turudi vijijini kuwekeza kwenye kilimo kulingana na zao la uchumi linalo stawi kwenye maeneo tutokako

mriringa

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2017
Posts
663
Reaction score
714
Ujana ni maji ya moto na uzee ni maji ya baridi na ikumbukwe uzee ni usiku.

Wakati natafakari maisha yangu huku nikiwaza kesho yangu imenilazimu niwaze mbali kwaani kuwaza karibu ni sawa na kuchimba shimo ndani ya nyumba.

Uzi huu najua wengi hatuupendi kwavile tunaona leo yetu kama kesho yetu ila ukweli ni kwamba kesho yetu ni ngumu kama leo hujaanda kesho yako.

Wakuu maisha ni fumbo ambalo Mungu pekee analijua na kama binadamu hatujui basi ni mda muafaka wa kuwekeza kwenye kilimo hasa cha mda mrefu ambacho utakula hata uzeeni( ikumbukwe nimesema maisha au uhai ni fumbo hivyo nawe ishi kwa fumbo kwaani hujui utaishi miaka mingapi na ili kuepuka msemo wa MAJUTO NI MJUKUU basi anza kupambana maana mjini kuzuri ukiwa na afya ila ukizeeka mjini kwa mto).

Wakati nawaza vijana kutoka Iringa na Njombe waliopo mjini miaka nenda rudi bila kurudi kuwekeza hata kwenye kilimo cha miti au parachichi huku maeneo ya familia yakiuzwa maana hayana mlimaji. Vijana TURUDI nyumbani tukawekeze ila maisha yawe mjini haina shida.

Miti inalipa sana ila utawala wa mwendazake ulikuwa mgumu kwa hilo zao ila sasa naamini supply na demand ya mbao au nguzo itakuwa kubwa sana.

Narudia kusema wapendwa tuwekeze kwenye ardhi na tulime kwa juhudi mazao ya mda mrefu maana hata uangalizi wake sio kazi ukilinganisha na mazao ya mda mfupi, lakini nisinukuriwe vibaya kwamba mazao ya mda mfupi hayafai hapana maana kuna baadhi ya mikoa hakuna mazao ya mda mrefu kama mikoa mingine.

Tucheze na fulsa zinazopatikana kwenye maeneo yetu. Kila lakheri kwa atakayeona Kuna sababu kuchukua wazo langu au ushauri huu.
 
Kuna rafiki yangu anamawazo kama hayo eti anarudi kijijini kufanya kilimo mtaji hana afya yake hovyo tu.......nime mwambia anatafuta kifo cha mapema kilimo kina wenyewe, kama sio basi uwe na mtaji wa kutosha, ukisikiliza maneno ya wana siasa eti kilimo ndo uti wa mgogo wa taìfa, wakati wenyewe wako Town.
 
Huyo kachelewa na huenda yupo kwenye kujutia. Kwa ukanda wa Iringa na Njombe kwa sasa hata ukirudi huna cha kufanya maana kule msimu wa mvua ukiwa na afya yako njema basi afya yako ndo mtaji. Msimu huu kule kama una miti mikubwa basi ni kipindi cha pruningi(prooning) lakini kama mpango wa kupanda au kulima haiwezekani. Mtie moyo usimkatishe tamaaa
 
Na ambao hawakuzaliwa kijijin warudi wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…