The BornAgain
JF-Expert Member
- Jun 23, 2024
- 428
- 582
Maisha yetu na safari nzima ya maisha ni Project yetu.
Madamu ni project mhimu kila mmoja ajifanyie SWOT analysis yake, hii itamsaidia ajitambue, ajirekebishe, ajitathmini na aamue mambo mbalimbali kwa ufasaha ili hatimae afikie malengo.
SWOT yako yani:
Strength zako: tambua mazuri au nguvu yako yenye kukusaidia kufanikiwa mfano afya, utimamu wa viungo vya mwili, nk. Vitu au mambo hayo ukiyatumia vema hakika utafikia malengo yako na makusudi ya kuumbwa kwako.
Weakness zako: yani tambua madhaifu yako mfano uvivu, kukosa maamuzi sahihi, imani haba, uoga, wasiwasi, ukosefu wa skills nk, kisha tafuta solution ya kuondokana au kupunguza madhaifu hayo maana ndio sababu ya wewe kurudishwa nyuma au kutofanikiwa ilivyo ktk maisha yako. Shughulikia madhaifu hayo kutegemeana nini chanzo cha dhaifu husika mfano kama ni ukosefu wa skills fulani..tafuta kujifunza, kama ni imani haba jaribu kuwaona watumishi wa Mungu, nk nk.
Opportunities: Yani fursa ulizonazo kwa maisha yako. Kila mtu kwa wakati fulani huwa na fursa mbele yake, kazi yako ni kuzitambua fursa around you. Fursa ni mambo au vitu vinavyoweza kutumika kukuinua kiuchumi, kiroho au kijamii. Popote ulipo inawezekana kuna fursa hujazitambua, ni mda sasa kuzitafiti uzijue kisha jaribu kuzitumia. Mfano fursa za elimu, mafunzo, imani, kazi, marafiki wazuri, sera nzuri za serikali , uwepo wa ajira mbalimbali, uwepo wa mikopo, nk nk.
Threats, yani vihatarishi: Jaribu kutambua au kuainisha vitu au mambo hatari kwako na ustawi wako. Mara nyingi vihatarishi havitokani nawewe ni mazingira ya nje kabisa, hivyo ni vema kuwa aware mara kwa mara ili visikuzuie kirahisi kutofanikiwa mfano magonjwa, yapo ya kuepukika na yasiyo ila unaweza wahi matibabu, tabia mbaya za watu wanaokuzunguka unaweza jikuta uko jela, kanuni na taratibu za nchi ukizikiuka inakula kwako, hali ya hewa mbaya inaweza athiri afya yako, shughuli zako nk, sera za ajira nk mfano uhitaji wa uzoefu kazini, nk nk.
MUNGU ATUSAIDIE SOTE TUNAPOTAFAKARI SWOT ZETU, NA HATA KAMA USHAFANYA..FANYA TENA NA TENA.