Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 872
SHUKA NAYO HII NI NZURI KWA KUJIFUNZA👇🏿👇🏿👇🏿
Maisha ni duara, maisha yana kila aina ya Raha na karaha Zake. Hivyo ukipata Bahati ya kuwa umesoma sana na kuwa na kazi kubwa sana au na fedha nyingi kuna jambo moja muhimu sana hupaswi kulisahau. Jambo lenyewe ni kuwa na marafiki wa aina Zote. Marafiki hao ni kama wafuatao:
1. Marafiki wasomi
Hawa ni muhimu kwa kukupatia urahisi wa kazi zako na connections za kutatua shida za kikazi . Kuwa nao karibu lakini kumbuka hawawezi kusaidia vitu vidogo vidogo. Mara nyingi wanakujaga msibani mkiwa mmeishazika alafu wanakaa nusu saa.
2. Marafiki wa Kazini
Hawa kuwa nao ili kazi ziende makazini lakini ndio hatari sana kwa wivu wakiona unafanikiwa. Mara nyingi hawa ukitoka Kazini ata simu hawapokei tena. Wanakugeuka kabisa Kama hawakujui . Ila Watumie Sana kufanikisha kazi zako Kazini
3. Marafiki matajiri
Hawa ni muhimu kuwa nao lakini uwe mvumilivu, hawaoni shida kukupoteza usiwe Rafiki . Ata ukikaa mwezi hujawatafuta wanaona Kama
Umekaa nusu saa. Ila akiwa na Shida yake kwako tegemea simu yake kutwa mara 6. Akikuahidi Mchango utafuatilia mwezi mzima alafu anakupa nusu ya ahadi.
4. Marafiki wa Shule
Hawa mliosoma nao hasa msingi na secondari. Mungu awabariki sana. Hawa wanakuwaga Kama ndugu zako. Ata Kama umesoma sana na una ukwasi hawakuogopi unless mwemyewe ujitenge. Wanaishi na wewe siku zote. Usiwapoteze hawa maishani mwako . Wanakopa kwa ajili ya urafiki
5. Marafiki wasio na uwezo
Hata ukiwa na wadhifa na Elimu gani, hawa marafiki wasio na uwezo na wasio na Elimu kubwa ni muhimu sana. Hawa wakija kwenye Shida yako inakuwa ya kwao. Wakati wale wasomi wanatuma Mchango kwa Simu, hawa wanashinda na wewe usiku na mchana kufanikisha jambo lako. Wanaacha kazi zao zote kwa ajili yako na wanaweza kupoteza ajira ili apate nafasi ya kuja kukuzika Rafiki yake ilihali huna msaada tena . Watunze sana hawa .Hawa ufalme wa Mbingu ni wao.
6. Marafiki wanafiki
Hawa wako kwenye Makundi yote. Huwezi kuwajua mpaka siku wewe ndio uwe unategemea kwake. Ndio utajua kumbe XYZ sio mtu siku hiyo. Utajua kuwa alikuwa na visa Moyoni kwake vikisubiri kulipiza. Hawa wamejaa laana na usipoteze muda wako kuwakumbusha ulichowatendea maishani mwao kwa kuwa ni agent wa ibilisi duniani
Life without friends is like life without sun
2022 chagua kuishi vyema na watu wa aina zote.